Ads

UJERUMANI NA TANZANIA NA KUBADILISHANA MALI NA VIFAA VYA KITAMADUNI VILIVYO CHUKULIWA NA WAJERUMAN MIAKA 100 ILIYOPITA



Na John Luhende 
mwambawahabari
Mkurugenzi wa makumbusho ya Taifa Profesa Andax Mabula amezindua mradi uliopewa jina la Humboldt Lab Tanzania utakaolenga ushirikiano wa karibu wa masuala ya makumbusho kati ya Tanzania na Ujerumani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo prof Mabula amesema lengo kuu la mradi huo nikupata maana ya vitu mbalimbali vilivyochukuliwa na wajerumani nchini miaka 100 iliyopita ikiwa pia kutakuwa na onesho maalumu ambalo litalenga zaidi kutoa taswira ya vita ya majimaji.

profesa Mabula amebainisha kuwa mradi huo uliozinduliwa nikwaushirikiano mzuri kati ya makumbusho ya  echnological ya Ujerumani na makumbusho ya taifa ya Tanzania ambapo pia kutakuwa na onesho maalum lililopewa jina la kuishi ndani ya simulizi.

Hatahivyo mshiriki aliyeshiriki katika utafiti uliofanywa wakati mradi huo unaandaliwa ambaye ni mkufunzi wa chuo kikuu cha dar es salaam Prof. Elias Jengo amesema nivyema watanzania wakaenzi na kutunza  vitu vyao ambavyo vinaonesha sura ya Tanzania miaka mingi iliyopita kwa faida ya vizazi vijavyo.

Naye dokta Lily Reyels ambaye ni msimamizi wa Humboldt Lab Tanzania na ujerumani anayeishi dar es salaam amesema kazi ya utafiti iliyo fanywa ninzuri na kubwa ambayo itatoa matokeo chanya katika maswala ya historia huku akibainisha kuwa mradi huo umefadhiliwa na serekali ya Ujerumani.

No comments