UJENZI WA DARAJA LA KIJICHI TUANGOMA KUANZA JANUARY 24/2017
Na John Luhende
mwambawahabari
Serikali ya Manispaa ya wilaya ya Tememe na kampuni ya Ujenzi ya China CRJE wametiliana saini mkataba wa Ujenzi wa Daraja litakalo unganisha eneo la kijichi na Tuangoma wilayani humo.
Akizungumza katika hafla hiyo mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Temeke ambaye pia ni katibu tawala Wilaya hiyo Hashim Komba , amesema daraja hilo linajengwa ili kuondo usumbufu wanaoupata wananchi wanaoishi maeneo hayo kwa kuzunguka Kigamboni na kongowe wakati wa masika.
Aidha afafanua kuwa Daraja hilo litakuwa na urefu wa Mita 800 na barabara za mitaa zaidi ya kumi zenye urefu wa Kilomita 1.8 na barabara nyingine zenye urefu wa kilomita 84 zote zitajengwa kwa kiwango cha lami na kitapimwa viwanja zaidi ya mianane kuzunguka eneo la mradi huo.
Naye mkurugenzi wa mradi huo wa kampuni ya Ujenzi CRJE Zhao Yefang ameshukuru kupewa kazi hiyo ana ameahidi kufanya kwa viwango kama walivyo jenga Daraja la Kigamboni watahakikisha ubora na thamani ya hela vinazingatiwa na ndani ya mwaka mmoja watakabidhi Daraja hilo.
Post a Comment