TEACHERS JUNCTION : TUNA WATAFUTIA KAZI WALIMU KATIKA MAZINGIRA WANAYOYATAKA (SIKILIZA AUDIO)
Na John Luhende
mwambawahabari
Ujira mdogo na mazingira magumu ya kazi nimoja ya mambo yanayo changia kushusha thamani ya mwalimu hapanchini teachers Junction nitaasi inayo jishugulisha na kazi ya kuongeza thamani ya mwalimu na kumtafutia kazi katika mazingira anayotaka kufanyia kazi na kiasi cha mshahara anaotaka kulipwa na imeonekana kuwa na mafanikio makubwa , na shule nyingi za private zimekuwa na mawasiliano ya karibu na taasisi hii kwakuwa hapa walimu huandaliwa kwa weledi mkubwa.
Njama salumu ni Afisa mradi wa Teachers Junction akizungumza na Mwambawahabari amewata walimu wa shule za msingi na sekondari kujiunga na kituo hicho ili kuboresha elimu zao kwa vitendo na kupata ajira kwa haraka.
"Tunao wataalamu wazoefu na wenye uwezo mkubwa wakutoa mafunzo kwa walimu, unajua walimu wengi wamaeandaliwa kufanya kazi katika mazingira ya shule za serikali wakienda kufundisha shule binafsi wanakuwa wanakosa baadhi ya vitu wakija kwetu tunawaongezea thamani kwa kuwapamafunzo ya ziada ambayo katika vyuo hawafundishwi na tunawatafutia kazi " alisema Njama
Aidha amesema changa moto kubwa inayowakabili waalimu ni ajira teachers Junction inatoa fursa
ya mafunzo kwa vitendo kwa walimu tunaomba wajitokeze kujiunga na kituo hiki ili wajihakishie kuwa na ajira.
Pamoja na hayo Njama ametaka serikali wanafunzi na jamii kwa ujumla kutambua na kuenzi kazi nzuri zinafanywa na waalimu katika kuelimisha Taifa.
"Hivikarbni kumekuwa na baadhi ya watu wakiwemo viongozi wa serikali na wanafunzi wanawadhalilisha walimu nadhani sijambo zuri waache wawaheshimu alisema Njama.
Post a Comment