TCRA YATAHADHARI WANANCHI KUHUSU UTAPELI WA MITANDAO.
Na Maria Kaira
Mwambawahabari
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)imewataadharisha wananchi wanaotumia huduma za mawasiliano nchini kuwa makini na utapeli unaofanywa na baadhi ya watu kwa kutumia simu za mkononi.
Akizungumza na waandishi wa habari Jiji Dar es Salaam Kaimu Meneja Mawasiliano kwa Umma TCRA Semu Mwakyanjala amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la matapeli wanaoghushi utaratibu wa mawasiliano na kutumia njia ya kuwalaghai na kuwashawishi watu Kutuma pesa kwa njia ya simu za mikononi.
Mwakyanjala ameutaka umma kutotekeleza maagizo yoyote yanayotokana na ujumbe wa simu za mkononi ambao utamtaka mwananchi kutuma fedha kutoka kwa mtumiaji asiyemjua.
" Utakapo pokea taarifa kwa njia ya simu au ujumbe wa maandishi kuwa umetumiwa Fedha kwa makosa na kutumiwa ujumbe mfupi unaofanana na ujumbe unaotumwa na watoa huduma na kukutaka urudishe fedha hizo usifanye haraka, tunakushauri uchukue tahadhari za kuweza kudhihilisha uhalali wa taarifa hizo, tena ikibidi uwasiliane na kituo cha wateja cha mtoa huduma wako " amesema
Pia ametoa wito kwa wananchi wote kutokutoa namba zao za siri au taarifa zao binafsi kwa mtu yeyote atakayempigia na kutaka taarifa zake, pia amewashauri wananchi kutoa taarifa kwa mtoa huduma wake na polis pindi anapopoteza simu au laini.
Post a Comment