Ads

TANZANIA YAWA MFANO WA KUIGWA BARANI AFRIKA MRADI WA MABASI YA MWENDO HARAKA( DART)




Na JohnLuhende 
mwambawahabari
Kutokana na Tanzania kufanikiwa katika sector ya usafitishaji hasa katika mradi wa Mabasi ya mwendo kasi  DART  ambao umeifanya kuwa nchi ya Tatu barani Afrika  baadhi ya nchi za Afrika zimevitiwa na mradi huo na kuamua kuja kujifunza mafanikio ya mradi huo.

Zimbabwe ni miongoni kwa nchi ambazo zime vutiwa na mradi huo , ambapo Waziri wa serikali za mitaa wa nchi hiyo Kasukuwere Savior amefanya ziara ya kutembelea mradi huo jijini  Dar es salaam  akiwa na Waziri wa serikali za mitaa (TAMISEMI).

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri huyo amesema  Zimbabwe imekumbwa na Changamoto  ya usafiri  ikiwemo foleni, amesema wanampango wa kuanzisha Huduma ya mabasi ya mwendo kasi (haraka) ili kupunguza msonga mano huo na  kuchochea maendele na ukiaji uchumi , wameona Tanzania ndiyo nchi pekee wanapoweza kujifunza mbinu hizo.

Naye Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI mhe.George Simbachawene amewataka watanzania kujivunia  mradi huo na kwamba Tanzania  iko tayari kufanya ushirikiano na nchi zote zinazo hitaji kujifunza uta alam na mbinu mbalimbali za mradi huo .Mradi huo ulizinduliwa  rasmi january 25 /2017 na  Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. John Pombe Magufuli

No comments