Ads

ONYESHO LA MAJIMAJI FLAVA KUTIKISA BAGAMOYO NA DAR



Na.John Luhende 
mwambawahabari
Flinn works(Kassel/Berlin) ya Ujeruman kwa kushirikiana na Asedeva ya  Dar es salaam Tanzania wameandaa onyesho la filam lenye lengo la kuelezea kihistoria kati ya ujerumani na Tanganyika  katika vita vya  maji maji  vilivyo piganwa mwaka  1905_1907 .

Akizungumza na waandishi wa habari  katika ukumbi wa  Makumbusho ya Taifa    Isaack Abeneko wa Asedeva, amesama wasanii  na wachezaji waliotengeneza kazi hiyo wana mitazamo tofauti ya kimsingi ya kisanii,kiutamaduni na siasa kama inavyo athiriwa na Jiografia  mitazamo hii haita funikwa itawekwa wazi  kwa  msisitizo  kwenye kuongoza  hatua ya namna ya utayarishaji kisanii.


Amesema Mambo ya kigeni yasiyokuwa ya kawaida yatapambanuliwa,fikra kandamizi na Mawazo yanayo kinzana vita pimwa na kuelezwa kisanii, pia mradi unaalika  mgongano wa mitazamo ya kuhusu tukio hilo na athari zake leo.   

Maji maji Flava ita tengeneza nafasi kisanii na kuifafanua katika lugha ya kiswahili,Kiingereza na Kijeruman, dhahania za kitamthilia zitagongana  pamoja na midundo na sayansi yenye kushangaza na ngoma za wakati huu zikiwekwa kwa pamoja na dhihaka.

Naye  Lisa Stepf wa Flinn works  amesema tukio hili litaelezewa kiunagaubagha ili vizazi ambavyo havikuwepo enzi hizo viweze kujua historia hiyo ambayo nimuhimu sana kwa nchi hizo mbili, na onyesho hilo limeanzia nchini Ujerumani katika miji  ya  Kassel na Berlin mwezi septemba na Oktoba mwaka 2015 na maonyesho yote 14 yaliyo fanyika   yalipokelewa kwa  mwitikio Mkubwa  na watazamaji.

Hapa nchini yatafanyika maonesho  TASUBA Bagamoyo 21/Jan/2017, Dar es salaam   International Academy 24January 2017,  na onyesho la mwisho ni tarehe 26 _28  January katika Makumbusho ya Taifa  Jijini Dar es salaam, na amewahiza watanzania kwenda kujionea maonyesho hayo.

No comments