Ads

MEYA WAJIJI LA DAR ES SALAAM AWATAKAWAKRISTO NCHINI KUIMBEA NCHI KUEPUKANA NA UKAME NA BAALANJAA.


Na Maria Kaira
Mwambawahabari
Wakristo wote nchini kwa pamoja wametakiwa kuiyombea nchi  kupata mvua ili kuondokana na ukame uliopo kwa lengo la kuepusha baa la njaa hapa nchi.

Wito huo umetolewa Leo hii na Meya wa Jiji la Dar es salaam,Isaya Mwita wakati akizungumza na waumini wa kanisa la KKKT Usharika wa Kijichi jijini Dar es Salaam .

Aidha Mwita amewaomba wanadar es salaam kila mmoja kwa imani yake kumuomba mwenyezi mungu aijaalie nchi ya Tanzania kupata mvua za kheri zitakazosaidia kuepusha ukame na madhara yake ikiwemo baa la njaa hapa nchi.


"Wanadar es salaam jambo tulilonalo mbele yetu tunawajibu wa kuomba mungu mvua zinyeshe kwa kiasi cha kawaida  ,ambacho hakitawe kuleta madhara yoyote kwa jamii ikiwa na kupunguza njaa hapa nchini.Mvua isipo nyesha katika uso wa dunia hii watoto wa mungu watateseka " amesema

Pia amewaomba kila mwanadar es salaam kutunza mazingira yanoyomzunguka kwa kuweza kuhifadhi takataka katika chombo maalum kwa lengo la kupunguza  magonjwa ya mlipuko katika jamii inayowazunguka.

Kwa upande wa muumini wa kanisa hilo Bw.Wistoni Mbuga amewahasa wanajamii wenzake kutunza mazingira kwa kupanda miti katika maeneo wanayoishi ili kuweza kuokoa na hali ya hewa iliyopo.

" kunaaja ya kuendelea kumuomba mungu maana tangu nimezaliwa kunamaeneo sijawahi kuona maji yamekauka, sasa unapoona maji hayo yanakauka ni jambo la kumlilia mungu atuepushe na janga la njaa linalokuja hapa nchini" amesema

Pia amempongeza meya huyo kushirikiana nao katika ibada takatifu iliyofanyika katika usharika wao wa kijichi na kumbusha wakristo wote kuungana na kumuomba mungu kuleta mvua nchini ili kupunguza baa la njaa.

No comments