MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE TANZANIA (TAWJA)
Na: Frank Shija
mwambawahabari
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA).
Hayo yamebainishwa na Katibu wa Chama hicho Jaji C. W. Makuru kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imesema kuwa imesema kuwa Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa mgeni rasm katika Mkutano Mkuu wa nanw wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) utakaofanyika kesho (leo) jijini Dar es Salaam.
Imeongeza kuwa mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa PSPF Goldeni Jubilee Tower ghorofa ya nne na unatarajiwa kuanza majira ya saa moja na nusu asubuhi kwa wageni waalikwa kuwasili na kujisajili.
Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa Mkutano huo utatanguliwa na mafunzo ya uandishi wa hukumu na elimu kuhusu mifuko ya jamii.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo mkutano huo unatarajiwa kuudhuriwa na wa wanachama ambao ni Mahakimu na Majaji 200 kutoka pande zote za Tanzania.
Kauli mbiu ya Mkutano huo ni“Ongoza njia katika kufikia upatikanaji wa haki kwa wakati na kwa wote”.
Post a Comment