MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE TANZANIA
Makmu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Jaji Mstaafu Engera Kileo(wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na baadhi ya Majaji na Mahakimu wakifuatilia mkutano mkuu wa nane wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa nane wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) wakiimba wimbo wa taifa jana jijini Dar es Salaam.
MH3a: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Amon Mpanju (kulia) walipokutana katika hafla ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) jana jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) Jaji Wambura jana jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya vitabu kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Kanda ya Tanga, Iman Abood wakati mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho jana jijini Dar es Salaam.
Jaji Kiongozi wa Mhe. Ferdinand Wambali akionyesha Tuzo aliyopewa na Chama cha Majaji Tanzania (TAWJA) kwa kutambua mchango wake katika kukiendeleza Chama hicho jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa TAWJA Mhe. Jaji. Iman Abood.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) jana jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto waliokaa ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Ramadhan Omary Makungu, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman, Mwenyekiti wa TAWJA Jaji. Iman Abood na Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Wambali.
Picha na Frank Shija – MAELEZO.
Post a Comment