Ads

HOSPITALI YA KIBITI YAPOKEA MSAADA WA VITANDA


Displaying IMG-20170127-WA0007.jpg

Na Maria Kaira 
Mwambawahabari
Hospitali ya Wilaya ya Kibiti imepokea msaada wa vitanda viwili vya kujifungulia wakina mama wajawazito kutoka katika hospitali ya taifa Muhimbili ikiwa na lengo la kuboresha huduma ya Afya  ya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Akizungumza na waandishi wa habari leo hii jijini hapa Muuguzi wa huduma za uuguzi na ukunga kutoka hospitali ya taifa Muhimbili Agnesi Mtawa  amesema kuwa wameguswa na kutoa msaada katika hospitali ya wilaya ya Kibiti baada ya kuona hospitali hiyo kuwa na uwitaji mkubwa na ukosefu wa vitanda vya kujifungulia wakina mama wajawazito .


Pia ametoa wito kwa hospitali ya kibiti kuangalia vitanda hivyo kwa umakini na pindi vitakapo pata itilafu yoyote wajaribu kuvitengeneza ili kuweza kuboresha vitanda hivyo ambapo vitaweza kuwasaidia wakinamama kupata huduma nzuri wakati wa kujifungua.

"Tulikuwa na vitanda 20 tulivyovifanyia marekebisho na sisi tukapata vitanda vingine vipya katika hospitali yetu tukaona sio vibaya tukivigawa vitanda hivyo katika hospitali zenye uwitaji ambapo vitanda 5 tuligawa katika hospitali ya Mafya, viwili tumetoa katika hospitali ya Wilaya ya Kibiti tumebaki na vitanda 13 hivi tutavigawa tena katika hospitali ambazo zinauwitaji" amesema

Hata hiyo Agnesi anawaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuchangia utoaji wa vifaaa katika hospitali yoyote ili kuweza kuboresha huduma za Afya na kupunguza vifo vya mama na motto.

Kwa upande wa Mhandisi  Ujenzi kutoka halmashauri ya Kibiti  Ayubu Ngereza ameshukuru uongozi wa hospitali ya Muhimbili kwa msaada wao walioutoa, pia amesema kupitia msaada huo utaweza kupunguza matatizo kwa akina mama pindi wanapotaka kujifungua katika hospitali hiyo.

"Tulikuwa  tunaupungufu wa vitanda katika hospitali yetu ila hivi tulivyovipata vitasaidia kwa kiasi chake ingawa bado tunauwitaji wa kupata vitanda vingine vya kuwasaidia wakinamama wakati wa kujifungua

No comments