Ads

( SIKILIZA AUDIO HAPO CHINI)WACHINA KUIBADILISHA ILALA KUWA YA KISASA


Displaying IMG_20161208_105506.jpg
Mkuu wa wilaya ya ilala mh sofia Mjema  mwenye kilemba cha bluu ,wakwanza upande wa kulia ni katibu tawala wa  wa manspaa wa ilala  Benard Mpogolo ,anayefuatia ni MSTAHIKI Meya wa manispaa ya ilala  Charles Kuyeko anayefuatia  ni bwana  Zang Ajun  na wakwakulia ni mkurugenzi wa manspaa ya ilala, wakiwa katika picha ya pamoja . (picha na John Luhende. )

Na.John Luhende
mwambawahabari
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema leo amekutana na ugeni kutoka nchi ya China Jimbo la Jiang Su, Manispaa ya xuzhou na kukubalina mambo mbalimbali yenyetija kwa maendeleo ya Wilaya ya Ilala.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam mh Mjema amesema kuwa ugeni huo unatija kwao kwani miongoni mwa mambo waliokubaliana ni kuipendezesha wilaya ya Ilala ifanane na maeneo mbalimbali ya nchini China kwa kuzingatia usafi wa maeneo husika, vilevile wamekubaliana katika suala la usalama kwa kupeana ujuzi wa kiusalamawanaotumia China ikiwemo  vifaa vya kisasa wanavyotumia kudhibiti vitendo vya uhalifu nakulinda miji yao.


Aidha  Mjema amesema kuwa suala la elimuhususani ya Sayansi kwa wachina watasaidia  kuchochea Tanzania ya Viwanda aliyokuwa anainadi Rais Magufuli kipindi cha kampeni za urais, na kusisitiza kuwa yapo maeneo mbalimbali kwa ajili ya uwekezaji.

Katika hatua nyingine mheshimiwa  Mjema ameeleza kuwa China ilikuwa sawa na Tanzania miaka 20 iliyopita lakini nidhamu na bidii ya kufanyakazi ndiyo imewapelekea kufika hapo walipo, hivyo amewaomba watanzania kuiga mfano huwa ili kufikia malengo yamapinduzi ya kiuchumi.

Kwa upande wake muwakilishi kutoka China ambaye pia ni  makamumwenyekiti wa kamati ya jimbo hilo   bwana Zhang Aijun amesema wapo tayari kushirikiana na wilaya ya Ilala na wataleta wataalaamu kuangalia fursa nyingine ambazo wanaweza kuwekeza kwa maendeleo ya pande zote mbili.




No comments