USAFIRI: Unaweza usiamini ila hivi ndivyo ilivyo
Na Leonard Mutani
mwambawahabari
Usafiri ni sehemu mojawapo ya kujongea kutoka sehemu moja na kuelekea sehemu nyingine huku chombo chochote kinachoweza kukusafirisha sehemu husika kwa lengo linalofanya kwenda hapo, hii ni sehemu ya maisha ya binadamu inayofanya neno usafiri kuwepo kwenye mfumo mzima wa maisha ya kila siku.
Mfano wa Safari za mwanzo kabisa kusafiri hapa Africa.
|
Hii inatokana na binadamu kukaa na kutafakari nini kifanyike kupunguza urasimu wa kupoteza muda wa kutembea, hata hivyo pamoja na kuwepo kwa mazingira ya kupunguza muda wa mtu kutoka eneo moja mpaka lingine, teknolojia ilileta chombo kijulikanacho kama pikipiki ya magurudumu mawili, hiki ni chombo kilichokuja kusaidia kupunguza muda na kuharakisha safari, kwa nchi za kiafrika imekuwa ni msaada mkubwa ikiwa na maana hata kule chombo kingine kisipoweza kufika kutokana na njia, ufinyu wa eneo pamoja na gharama, basi chombo hiki kinaweza kufika kwa wakati na kwa garama ya chini.
Hii ni baada ya harusi, safari inaanza.
|
Hata hivyo uwepo wa chombo hiki hususani hapa nchini umekuwa na faida na hasara zake kutokana na matumizi yanayotumika tofauti na watengenezaji wake hama sheria za nchi kinapotumika.
Hapa nchini kumekuwa na baadhi ya waendesha pikipiki hizo maarufu (Bodaboda) wakitumia chombo hicho tofauti na uwiano mahususi, kutokana na hilo waendeshaji wengi hama abilia waliowahi kubebwa wamebaki hawana moja ya kiungo cha mwili kutokana na ajali iliyotokea kutokana na kutofuata utaratibu unaopaswa, hivyo kupelekea makosa na maumivu kwa mhusika.
Hapa chini tumekuwekea picha kadhaa zikionyesha moja matumizi yasiyo sahihi kwa pikipiki ya magurudumu mawili iliyoweza kubeba abilia na muendeshaji wake kufikia watu sita (6), hapo ni eneo la Mbagara Kisewe, ambapo ilipouliza kwa vijana wengine ambao walishuhudia hali hiyo tulipata hili hapa,
“kaka hali hii sisi wenyewe hatuipendi ila inatokana na abilia mwenyewe anakuja na wenzanke kama unavyoona anakwambia tunaenda sehemu fulani tuna shs 1000/- ukiangalia bosi anasubili hesabu na sehemu wanapokwenda siyo mbali basi unawapelekea hivyo hivyo tu” alisema Mohamed mmoja wa waendeshaji wa bodaboda wa eneo hilo.
Hii ni pikipiki inayoruhusiwa kubeba watu wawili lakini hapa imeweza kubeba watu sita kwa mara moja kitu ambacho si kawaida.
|
Mpita njia akipita karibu na pikipiki iliyobeba watu sita, kupitia picha hii ndipo unaweza kuwaona wote waliobebwa, mbele ni (1) kijana mdogo, anayefuatia ni (2) dereva wa pikipiki hiyo, nyuma yake kuna (3) binti mdogo kavaa ushungi wa bluu,anayefuatia (4) mwenye kilemba cha njano kuna (5) mtoto wa kike anaonekana kichwa ambapo wa mwisho ni (6) dada mwenye ushungi mwekundu na ameshika kikapu.
|
Post a Comment