Ads

UNICEF YAADHIMISHA MIAKA 70,MAFANIKIO YAKE KATIKA KUTETEA WATOTO NCHINI YABAINISHWA


Displaying _MG_1152.JPG
Rais wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana mh Ali Hassan Mwinyi  wapil upande wa kushoto akizungumza katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 70 ya UNICEF wakwanza upande wa kushoto ni mwakilish wa UNICEF Maniza Zaman,wakwanza kulia n mwakilish wa UNICEF Alvaro Rodriguez, na wapili kulia ni waziri wa Afya  maendeleo ya  jamii, jinsia, wazee na watoto mh Ummy Mwalimu, wakifuatilia hotuba.


Na Maria Kaira
mwambawahabari
Asilimia 90 ya watoto  Nchini wamepata vyeti vya kuzaliwa tofauti na hapo mwanzo ambapo ili kuwa haizidi Asilimia 20 ya watoto kupata kupata vyeti hivyo.

Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo linalo simamia  haki za watoto UNICEF zilizofanyika katika ukumbi wa Mwalimu nyerere Jijini Dar es salaam, Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto  mh Ummy Mwalimu amesema zoezi hilo limewezekana  katika mikoa ya Njombe,Iringa,na Mbeya.

Hata Hivyo Waziri Ummy amesema shirika hilo la UNICEF limetoa msaada  Mkubwa nchini ikiwa ni pamoja na kulinda usawa kwa watu walio adhirika na uginjwa wa Ukimwi,watoto wenye udumavu,kukomesha na kuwa saidia watu walio adhirika na homa ya Dengue Nchini.


Hata Hivyo mwakishi wa shirika hilo la UNICEF Tanzania Maniza Zaman amesema anamshukuru sana Raisi  Mstaafu wa Tanzania Alhasan Mwinyi kwa kukubali kusaini Mkataba wa ushirikiano wa Tanzania na Shirika hilo lililo anzishwa mwaka  1990 kwani kwa kisaini kwake ndio kumeleta matokeo ya ukombozi wa haki za mtoto Leo hii.

Aidha Raisi  Mstaafu wa jamuuli ya muungano wa Tanzania Alhasan Mwinyi amedhihirisha kuwa hajutii kusaini Mkataba wa Tanzania kuwa wanachama wa UNICEF kwani kusaini kwake kwa Sasa watoto wanabahati ya kulidwa na kutetewa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Pamoja na hayo Msimamizi wa Umoja wa Mataifa UN katika shirika la UNICEF Alvaro Rodriguez ameongeza kwa kusema kuwa mchango wa shirika hilo la watoto ni mkubwa,Muhimu na wenye dhamani katika dunia ya Leo na ya kesho kwani wamefanikiwa kuwapa watoto waliokata tamaa sura za mafanikio na furaha .

No comments