Ads

UHAMIAJI DAR YANASA WASICHANA WAKIGENI WAKIENDESHA BIASHARA YA UKAHABA



Mwambawahabari
Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imewakamata wasichana 13 kutoka nchi za Nepal na India wenye umri kati ya miaka 18 na 26 ambao wameletwa nchini kinyume cha sheria na kujihusisha na biashara ya ukahaba.

Akizungumzia operesheni maalum ya kufunga madanguro na kusaka raia wa kigeni wanaoishi nchini kinyume cha sheria Kamishna wa Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam (RIO) John Msumule amesema Wilaya ya Kinondoni inaongoza kwa kuwa na madanguro mengi ikifuatiwa na Ilala ambapo kwa sasa wanajipanga kuyaondoa katika siku 10 zijazo.


Amesema, katika operesheni hiyo pia wamemkamata Bw. Mohamed Shabani Magamba kwa tuhuma za kutengeneza vibali vya kugushi vya kuwawezesha raia wakigeni kuishi nchini ambapo pia amekutwa na hati 4 za kusafiria za raia wa Nigeria, Botswana, Somalia na Uingereza.

Kamishna Msumule,, amewataka wamiliki wa nyumba kuhakikisha wana watambua wapangaji wao pamoja na kuwa na picha zao, na kuwaonya wale wanaoajiri raia wa kigeni bila vibali, kuoa ama kuolewa na raia wa kigeni asiye na vibali kufika katika ofisi za uhamiaji na kufuata utaratibu wa kisheria wa kupata vibali kabla hatua kali za kisheria azijachukuliwa dhidi yao

No comments