MKUTANO WA USHIRIKIANO WA KOREA NA AFRIKA KUFANYIKA ADDS ABABA
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari. Katika mkutano huo Bi. Kasiga aliwaeleza Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa Nne wa Mawaziri wa nchi za Afrika na Korea utakaofanyika Mjini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 06 na 07 Desemba, 2016. Mkutano huo utajadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Afrika na Korea pamoja na maeneo mapya ya mashirikiano.
Na Maria Kaira
mwambawahabari
Tanzania inatarajia kushiriki mkutano wa nne wa mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Korea utakaofanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika, Addis Ababa nchini Ethiopia Desemba 6 hadi 7.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakisikiliza na kunukuu kwa makini mkutano uliokua ukiendelea
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mindi Kasiga amesema mkutano huo umeandaliwa na serikali ya Korea kwa kushirikiana na umoja wa Afika ukiwa na lengo la kukuza ushirikiano na kuandaa maeneo mapya ya ushirikiano baina ya Korea na mataifa ya Afrika katika miaka mitatu ijayo.
Mindi amesema Tanzania ni moja ya nchi nne za Afrika ambayo Korea imezichagua kuanzisha mahusiano ya kimkakati yatakayozifanya nchi hizo kupewa kipaumbele katika kupokea msaada na mikopo nafuu kutoa Korea katika kipindi cha miaka mitano.
" katika kipindi hicho Tanzania itaweza kupokea kiasi cha Dora za kimarekani milioni 300 sawa na asilimia 17.1 ya msaada utakaotolewa barani Afrika na kufanya Tanzania kuwa nchi inayoongoza barani Afrika kupokea misaada kutoka Jamhuri ya Korea" amesema
Pia Mindi amesema nchi ya Tanzania imeweza kufaidika na miradi mbalimbali tangu kuanzishwa kwa mikutano hiyo ikiwa ni pamoja na mradi wa kuendeleza kilimo cha Mwani Zanzibar wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 3.6 na huduma ya uchaguzi wa Afya ya uzazi jijini Dar es salaam wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni nne.
Aidha aliongeza kuwa Jamhuri ya Korea imeazimia kushirikiana na Tanzania katika ujenzi wa mradi wa daraja la Kikwete kwenye mto Malagarasi mkoani Kigoma na hospital ya mama na mtoto iliyopo chanika jijini hapa.
" Ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano wa Afika na Korea utakuwa na fursa muhimu ya kukuza mahusiano baina ya nchi zetu mbili hususani katika nyanja za uchumi,pia Tanzania itatumia fursa hiyo kuiomba Korea kuongeza kasi ya utendaji wa miradi mipya ikiwemo mradi wa Daraja la Srlander ambao unatarajiwa kuanza mwaka 2017 na kukamilika 2020" amesema
Post a Comment