Ads

MKALI WA MASHAIRI KATIKA SHINDANO LA MEYA KUJULIKANA KESHO



Na,Maria Kayira 
mwambawahabari
Fainali  ya pili ya tunzo ya ushairi ya mstahiki meya wa jijini la Dar es salaam Isaya Mwita imefanyika leo Disemba 17, 2016 ikiwa na lengo la kuenzi historia ya Meya wa kwanza barani Afrika Abeid Amiri Kaluta ambaye pia alikuwa mshairi na kuweza kuibua vipaji vya watunga mashairi.

 Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa shindano hilo Chata Michael amesema kuwa mshindi wa tunzo hiyo atatangazwa kesho, pia amesema tunzo hizo zitakua endelevu kwa kupitia shindano hilo wataweza kujadili changamoto na maendeleo yanayojitokeza katika jiji la Dar es Salaam.



Aidha Michael amesema wameandaa shindano hilo ili kuweza na kuibua vipaji vya wasanii  na kukuza taaluma ya ushairi sambamba na wanataaluma wake kujitambua kwa kuweza kuienzi lugha ya Kiswahili hapa nchini.

 “Washiriki kwa mwaka huu wamejitokeza kwa wingi kuliko shindano lilipita tunaona watanzania wamelipokea vizuri, tumeandaa zawadi kwa  washairi watakaofanya vizuri,ambapo tumepanga kuchukua mashairi ya washairi watakao fanya vizuri na kuweza  kutengeneza vitabu vya ushairi vitakavyotumika katika shule za hapa nchini”

Pamoja na hayo Profesa Tigiti Sengo amewataka vijana hapa nchini kujikita zaidi katika kujifunza lugha fasaha ya Kiswahili, huku akiwataka walimu kukaa chini na kuweza kutengeneza tena mtahara sahihi ya lugha ya Kiswahili.

“Tupende lugha yetu wenyewe na tujikite hasa kujifunza kwa wanaojua lugha  vizuri ili lugha yetu izidi kuendelea”amesema

No comments