MEYA WAJIJI LA DSM ISAYA MWITA AZITAKA KAMPUNI ZA MAEGESHO JIJINI KUTOWANYANYASA WATEJA WA MAEGESHO
mwambawahabari
Na John Luhende
Kutokana na makapuni yaliyo pewa zabuni ya kusimamiashughu za Maegesho ya magari kuendelea kukiuka masharti na taratibu za jiji Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita,ameamua leoametoa ufafanuzi pamoja na tahadhari kwa makampuni ambayo yamepewa kazi hiyo
Akizungumza na Waandishi wa habari amesema kuwa ameamua kutoa ufafanuzi juu ya wafanya biashara hao ambao wamekuwa wakikeuka taratibu na kuanza kutoa tozo kubwa ya ushuru kwa watu ambao wamekuwa wakiegesha magari na kupandishiwa kodi kwa dakika chache pamoja na kukamata magari hayo na kuyafunga kamba.
“Ni kweli nimesikia habari hizo na ndo maana nameona niongee nanyi wanahabari hivyo naonya mawakala hao wanaofanya kazi kinyume na utaratibu huo na sasa naangiza kuwa mtu atakaye park gari anatakiwa gari likae dakika 60 bila kusumbuliwa na kama wataendelea kukiuka tutawafutiya lesseni ya kufanya kazi”amesema Mwita
Amesema kuwa ifikapo Januari,2017 kwa Makampuni yote kuanza kutumia tiketi za kielektroniki na kama kuna mawakala au kampuni watashindwa kutumia hizo tiketi watavunjiwa mikataba na pia anawataka watu lazima wadai tiketi hizo.
Pamoja na hayo Meya amesema kuanzia sasa anawataka mawakala kuanza kuwatoza watu ushuru kuwaacha wateja wao wapark dakika 60 ndipo wapewe Listi ya kuegesha magari huku wakitumia tiketi za Kielektroniki na mtu asipopewa listi hizo au kupandishiwa kodi wanatakiwa watoe taarifa kwa jiji la Dar es salaam.
Post a Comment