Ads

MAUZO KATIKA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM ( DSE) YAPANDA MARA 6.


Image result for logo ya dse

Na Maria Kaira
mwambawahabari
Mauzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yamepanda mara 6 zaidi kutoka Tsh.198 Millioni wiki iliyopita na kufikia Tshs 1.22 billioni wiki hii iliyoishia tarehe 9 Desemba, 2016.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Masoko Mwandamizi wa DSE, Marry Kinabo wakati akitoa ripoti yake ya mauzo ya soko hilo amesema pia idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa katika wiki iliyopita imeongezeka kwa 44% kutoka hisa 262,598 wiki iliyopita hadi hisa 378,149 wiki hii.


Pia Kinabo amesema ukubwa wa Mtaji wa Soko wa makampuni kwa ujumla ulishuka kwa asilimia 0.5% kwa makampuni ya ndani na umeendelea kubaki kwenye kiwango kile kile cha Trilioni 8.

Hata hivyo viiashiria katika sekta ya viwanda amesema imeshuka kwa pointi 104.63 wakati Sekta ya Huduma za Kibenki na Kifedha ikishuka kwa pointi 3.66 huku Sekta ya Huduma za Kibiashara wiki hii ikiendelea kubaki kwenye wastani ule ule wa TZS 3,157 sawa na wiki iliyopita.

No comments