MAHAFALI YA 9 YA CHUO CHA KODI YA FANA , WANAFUNZI 550 WAHITIMU
Mmwambawahabari
Msajili wa Hazina Dkt Osward Mashindano ameutaka uongozi wa chuo cha Kodi nchini kuongeza uwezo wa kutahini wanafunzi wengi ili kuiboresha fani ya kodi na forodha pamoja na utafiti wa masuala ya kodi katika sekta zinazokua kwa kasi kama ya uchimbaji madini mafuta na gesi ili kukuza uchumi wa nchi kwa njia ya makusanyo ya mapato katika sekta hizo
Ameyasema hayo katika mahafali ya tisa tangu kuanzishwa kwa chuo hicho ambapo wahitimu wa ngazi ya Cheti, Astashahada na Stashahada ya Uzamili katika Ushuru wa Forodha ya Afrika Mashariki zaidi ya 550 wamehitimu.
Aidha amesema amefahamishwa na uongozi wa chuo hiko kuwa kimejiimarisha katika nyanja za ushauri na utafiti ambapo mmeweze kutambulika nje ya nchi kwa kutoa huduma katika fani ya kodi na forodha," amesema na kuongeza.
"Ni matumaini ya serikali kwamba nyote mliofuzu mtajiunga na kundi la wataalamu wa forodha na kodi na kutumia ujuzi mliopata kwa faida ya taifa letu na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa kodi au kwa kuwasaidia walipa kodi kutimiza wajibu wao kwa kulipa kodi kwa hiari kama sheria kanuni na taratibu zibavyosema,"
Pia Dkt. Mashindano amesema Serikali na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) itaendelea kutoa msaada katika chuo hicho kwa ajili ya upatikanaji wa fedha utakaosadia kuwezesha mpango kazi wa chuo hicho.
Mkuu wa Chuo cha Kodi, Profesa Isaya Jairo amewataka wahitimu wa chuo hicho kuwatumikia watanzania kwa haki pamoja na kuhakikisha wanawapa elimu ya kulipa kodi ili wawe na mwamko wa kulipa kodi kwa hiari.
"Wahitimu ni wajibu wao kuwatumikia wananchi kwa haki pamoja na kuhakikisha wanatoa elimu ili walipe kodi kwa hiari," amesema.
Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere amewataka wahitimu hao kuitumia elimu waliyopata kwa kuisadia serikali kukusanya kodi na si kuwasadia wakwepa kodi kukwepa kulipa kodi.
Hata hivyo amesema wataalamu 558 waliohitimu wamekua ni jeshi kubwa sana, amewataka wakawe mabalozi kwa wenzao kwa kusaidia na kuweza kutatua changamoto zilizopo kwenye mfumo wa kodi pamoja na mikataba ya forodha na kanuni za usimamizi wa kodi kulingana na sheria za kodi za nchi.
Post a Comment