Ads

MAGAZETI YANAYO TUMIA PICHA ZA BLOG BILA IDHINI YA MWENYE BLOG KUKIONA





Mwambawahabari
Kaimu mweneyekiti wa muda wa chama cha Bloggers Tanzania Joachim Mushi (aliyesimama) akiongea wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi (kushoto aliyekaa)Mkurugenzi wa Habari Maelezo Hassan Abass wakati wa kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama.
Mkurugenzi wa Habari Maelezo Hassan Abass akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa waandishi wa habari kwa mitandao/bloggers wa chama pamoja na mafunzo.



Wanachama na waandishi/bloggers wakimsikiliza Maxence Melo kulia alipokuwa anatoa maelezo juu ya sheria inavyoweza kutumika pamoja na wasomaji wa mitandao hiyo wanachotaka kutoka kwa media yako.
Samwel Malecela (Le Mutuz Nation) ambaye ni mmoja kati ya waandishi wa mitandao ya jamii ya Le Mutuz Nation akitoa mawazo juu ya serikali kuwa wazi katika utoaji wa taarifa zake ikishirikisha waandishi wa media kama Bloggers.

Picha ya pamoja baadhi ya waandishi/wamiliki ambao ni bloggers wakipiga picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa habari maelezo Hassan Abbas aliyekaa mstari wa katikati aliyevaa kaunda suite. 
Picha zote na Leonard Mutani.

Chama cha wamiliki wa bloggera nchini Tanzania wamefanya mkutano mkuu wa mwaka 2016 wenye lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazohusu mitandao ya kijamii, uendeshaji na uandishi katika mitandao kwa ujumla.

Katika mkutano huo ambao mgeni  rasmi aliyefungua mafunzo hayo ya siku mbili yaliyofanyika jijini Dar es Salaam na mkurugenzi kutoka Habari Maelezo Dkt Hassan Abass ambaye amesema kuwa bloggers ni chombo rasmi cha habari kama vilivyo vyombo vingine vya habari na watu zaidi ya bilioni 3.5 duniani wanalishwa habari kwa sehemu kubwa kupitia chombo hiki.

Pia amesema ili habari iweze kuwafikia jamii kwa haraka, mara nyingi wanatumia waandishi wa mitandao (bloggers) kwani ni chombo cha habari namba moja, hivyo ameongeza kuwa serikali kwa sasa inatambua waandishi  kwa njia ya mtandao.

Amewataka bloggers kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya habari, kwa ukweli na usahihi, huku wakitabua kuwa bado wanachokiandika kinaleta manufaa kwa jamii nzima na ndipo jamii itaendelea kuwaheshimu zaidi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa muda wa chama cha bloggers nchini Tanzania Joakimu Mushi amesema kauli mbiu ya mkutano huo ambayo ni”mitandao ya kijamii ni ajira itumike kwa manufaa”amewataka wanachama wote kuweza kujikita kutoa habari na kujikita kutambua chama kama sehemu ya nafasi katika utendaji wa kila siku.


Dkt. Hassan Abass amesema;“kuanzia sasa  chombo chochote cha habari hususani magazeti yanapotumia picha hama habari iliyotoka kwenye mtandao wa kijamii kama (blogs) pasipo idhini ya mwenye mamlaka nayo kusitisha mara moja hama sheria ya hakimiliki itatumika"

No comments