VIJANA ZAIDI YA ELFU TATU NCHINI KUFAIDIKA NA MRADI WA RED TO WORK
![]() |
Badhi ya vijana waliojitokeza katika chuo cha usimamizi wa Fedha IFM,wakifanya usajiri kuingia katika mafunzo ya mradi wa Ready to work. |
mwambawahabari
BANK ya Barcrays Tanzania kwa Kushirikiana na shirika lisilo la
kiserikali la Junia Achievement wameanzisha mradi uitwao (Red to work) kwa Vijana
zaidi ya elfu 3 waliopo vyuoni .
Akizungumza na Mwamba wa habari wakati wa zoezi la uendeshaji wa mradi
huo katika chuo cha fedha (IFM) mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Hamisi
Kasongo amewataka Vijana kuchangamkia fursa hiyo pale watakapofika vyuoni mwao.
Amesema mafunzo ya red to work yatahusisha vyuo vya UDSM' IFM, TIA, CBE,
UDOM, CHUO CHA KODI, MZUMBE , pamoja na MWALIMU NYERERE kwa ajili ya kupata
ujuzi wa aina mbalimbali.
"Vijana wanatakiwa kutumia simu zao za
mkononi kulog in program ya bank ya bacrays ili waweze kuingia online kwa
urahisi kama watakavoelekezwa ili kupata fomu na kuweza kuijaza pamoja na
kuanza mafunzo.
Ameongeza kuwa Vijana watakapo maliza mafunzo ya ujuzi wa kuweza
kujiajiri, kutumia fedha zao vizuri, kulinda soko lake la ajira pale
atakapojiajiri na kuajiriwa atakuwa mzalendo
Mafunzo hayo yataendesha kwa njia ya mtandao, kwa siku 90 ambapo mhitimu
wa mafunzo hayo atatunikiwa cheti cha kimataifa kwa ushiriki wa mradi huo na
ujuzi wa aina nyingi katika kulijenga taifa.
Post a Comment