Ads

UJENZI WA RELI YA KISASA YA STANDARD GAUGE WAANZA




Na Maria Kaira 
Mwambawahabari
Ujenzi wa reli mpya  ya kati ya kisasa kwa kiwango cha (Standard Gauge) yenye urefu  wa kilomenta za mraba 1,219 inayokadiriwa kugharimu sh. Bilioni 3.694 kutoka Dar es salaam-Isaka-Mwanza imeanza kujengwa na itachukua muda wa miaka mitatu kukamilika.

Hatua hiyo ni moja wapo ya kutekeleza mkakati wa taifa wa maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2016/2017-2020/2021.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi mtendaji Masanja Kadogosa amesema utekelezaji huo umegawanyika katika awamu nne ndogo ambapo awamu ya kwanza ndogo itakuwa Dar es salaam- Morogoro km 202,awamu ya pili ndogo itakuwa Morogoro- Makutupora km 344, awamu ya tatu ndogo Makutupora-Tabora 294 na awamu ya nne ndogo itakuwa Tabora - Mwanza km 379.

Kadogosa amesema ujenzi wa mradi huo mkubwa wa kwanza nchi Tanzania utaleta maendeleo kwa haraka katika sekta ya kilimo, biashara, madini na viwanda hasa maeneo ambapo reli hiyo itapita na hata kwa nchi za jirani ikiwemo Rwanda, Burundi, Uganda, DRC na Kenya.

"Ujenzi wa mtandao mzima wa reli nchi unaotegemewa kujengwa kwa kiwango cha Standard Gauge utakuwa na jumla ya Km 2,561 na unatarajiwa kugharimu dola za marekani sh. Bilioni 7.683 ambapo utatekelezwa kwa awamu mbalimbali " amesema

Pamoja na kukamilika kwa mradi huo wa reli ya kati utaweza kuleta manufaa mengi ya kiuchumi na kijamii pia utaweza kusaidia kuboresha na kuunganisha usafirishaji kwa nchi zisizokuwa na bandari kuelekea masoko ya afrika na dunia kwa ujumla.

Hata hivyo kadogosa amesema mradi huo utavutia uwekezaji katika maeneo ambayo mfumo huo wa reli utapita, utaboresha usafiri wa reli ya kati na utaweza kuchochea maendeleo ya shughuli za madini na usafirishaji wa bidhaa Nje ya nchi.

No comments