Ads

MEYA ILALA ABORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU BONYOKWA


Mstahiki Meya Charles Kuyeko akiwa katika picha na vijana washule ya msingi Bonyokwa  walio fanyavizuri katika mtihani wataifa wa darasa la saba mwaka huu wote walipata daraja A,wote amewa ahidi kuwapa lakimoja moja kila mtu (picha na John Luhende) 
Mwambawahabari
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Bonyokwa Mhe. Charles Kuyeko leo tarehe 14/11/2016 amezindu madarasa matano (5) yaliyojengwa chini ya uwezeshaji wake kwa gharama ya Tshs. 85,000,000/=.

Meya Kuyeko pia amekabidhi madawati 250 kwa ajili ya Shule ya msingi Bonyokwa na kumaliza kabisa tatizo la wanafunzi kukaa chini.

Mwalimu mkuu, ndugu Davis Sanga ameelezea historia ya shule hiyo amesema kuwa ''Shule ya msingi Bonyokwa ilijengwa mnamo 01/01/2003 chini ya mpango wa MMEM ikiwa na wanafunzi 62 ambapo kwa inawanafunzi takribani 1200. Mwalimu mkuu pia ameelezea changamoto zinazoikabili shule hiyo kwa sasa ni ofisi ya walimu  na upungufu matundu ya vyoo 35.


Akijibu Risala hiyo Meya Kuyeko ameahidi kuanza kujenga madarasa mengine mawili kabla ya Desemba mwaka huu. Pia ameahidi kujenga matundu ya vyoo 20 , matundu 8 kwa wanafunzi wa kiume, matundu 10 wanafunzi wa kike na matundu mawili kwa ajili ya walimu na ofisi moja ya walimu.

Aidha Meya pia amewaahidi wananchi wa Bonyokwa kuwajengea shule ya Sekondari ya Kata kwa kuzingatia Bajeti/mwaka wa Fedha 2016/2017.

Katika kuhakikisha wanafunzi wanashiriki michezo Kuyeko amesema, atauboresha uwanja uliopo kwa kuwa ni mali ya shule hiyo, huku akiahidi kuwatafutia kiwanja kingine cha michezo kwaajili ya wananchi.

Kuhusu suala la ulinzi wa shule hiyo Diwani huyo amesema anampango wa kuweka uzio mwakani baada ya kuwashirikisha wananchi wa kata hiyo pamoja na wadau wa maendeleo.

Meya Kuyeko amewapongeza walimu, wazazi, kamati ya shule na wanafunzi wa shule hiyo  kwa kila mmoja kwa nafasi yake kutimiza majukumu yao. Meya pia alipata nafasi ya kushikana mikono na wanafunzi wanne waliofanya vizuri katika mtihani wa mwisho wa Darasa la saba na kupata wastani wa A. Meya Kuyeko aliwapongeza wanafunzi hao kwa kuwapa zawadi  ya fedha kiasi cha 100,000/= kwa kila mmoja.

No comments