Ads

Jamii yaaswa kufanya kazi kwa uaudilifu ilikujijengea heshima.

Displaying TZ1.JPG
Mhadhama Kardinali Polycarp Pengo na Dkt. Fredrick Kigady wakifuatilia historia fupi ya Tuzo ya BENEMERENTI ambayo upewa mtu aliyetoa mchango wake mkubwa katika kutumikia jamii pamoja na kanisa wakati wa hafla ya kumkabidhi tuzo hiyo Dkt. Kigadya mapema wikiendi hii Jijini Dar es Salaam.    

Displaying TZ2.JPG
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akizungumza katika hafla fupi ya kumkabidhi tuzo na kumvisha nishani Dkt. Fredrick Kigadye aliyotunukiwa na Baba Mtakatifu Papa. Francis  mapema wikiendi hii. Kushoto ni Mhadhama Kardina Polycarp Pengo, Dkt Fredrick Kigadye na Mkewe.

Displaying TZ3a.jpg
Mhadhama Kardinali Polycarp Pengo akimkabidhi hati yenye ujumbe maalumu kutoka kwa Baba Mtakatifu Papa. Francis Dkt. Fredrick Kigadye wakati wa hafla ya kumkabidhi tuzo aliyetunukiwa kufuatia mchango wake mkubwa katika kulitumikia Kanisa Katoliki kupitia Idara ya Afya chini ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) mapema wikiendi hii. Kulia ni Mke wa Dkt. Kigadye akishuhudia tukio hilo.

Displaying TZ3b.JPG
Mhadhama Kardinali Polycarp Pengo akimvalisha nishani ya heshima ijulikanyao kwa jina la  Benemerenti (Anayestahili) Dkt. Fredrick Kigadye aliyetunukiwa tuzo hiyo na Baba Mtakatifu Papa Francisco kufuatia mchango wake mkubwa katika kulitumikia Katisa Katoliki kupitia Idara ya Afya chini ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) jana Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mke wa Dkt. Kagadye akishuhudia tukio hilo.

Displaying TZ4.JPG
Dkt. Fredrick Kigadye akitoa neon la shukrani kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kwa kutambua mchango wake katika jamii na kanisa kwa ujumla.
Displaying TZ5.JPG
Katibu Mtendaji wa Baraza la Maaskofu  wa Katoliki Tanzania (TEC) Padre Raymond Saba akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Fredrick Kigadye wakati wa hafla ya kumkabidi tuzo mapema wikiendi hii Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Mpiga Picha  Wetu.
Na: Frank Shija,
Jamii imeaswa kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu, weledi na uzalendo wa hali ya juu ili wapate kuheshimika na kuthaminiwa na jamii zinazowazunguka kwa kutambua mchango wao katika kuendeleza jamii.
Hayo yamesemwa na Mhadhama Kardinali Polycup Pengo wakati wa hafla ya kumkabidhi nishani ya Benemerenti  (Anayestahili), Dkt. Fredrick Kigadye, ambayo utolewa na Baba Mtakatifu kwa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kulitumikia Kanisa na jamii kwa ujumla jana Jijini Dar es Salaam.
“Ni vyema tukatambua ya kwamba kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ndiyo msingi mkuu wa mafanikio mahali pepote pa kazi na katika maisha yetu ya kila siku”. Alisema Kardinali Pengo.
Kwa upande wake Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa masema kuwa Dkt. Kigadye amekuwa mtumishi wa wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kwa muda wa miaka 35 huku akifanya kazi katika Idara ya Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa mafanikio makubwa.
Ameonesha ni namna gani watu tunapaswa kujitoa kwa ajili ya kumtumikia Mungu kupitia vipawa na taaluma tulizo jaaliwakuwa nazo hii inatia moyo sana. Aliongeza Askofu Ngalekumtwa.
Akizungumzia Tuzo hiyo aliyopewa na Baba Mtakatifu Papa Francis, Dkt Kagadye amesema kuwa anajisikia mwenye furaha kubwa na wathamani kwa kupewa tuzo ya heshima na kiongozi mkubwa duniani nakuongeza kuwa tuzo hiyo inamuongezea chachu ya kuishi katika misingi imara ya maadili na weledi.
Aidha alitumia fursa hiyo kutoa raia kwa watanzania wengine hasa walei wa Kanisa Katoliki kutekeleza majukumu yao kwa kujituma zaidi ili kuwahudumia wana jamii wanaohitaji huduma za kanisa ikiwemo elimu, afya na nyingi nyingi.
Dkt. Fredrick Kigadye amekuwa mtanzania wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo baada ya  BABA Mtakatifu Fransisko kukubali maombi ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ya kumtunuku tuzo ya heshima aliyekuwa mkuu wa idara ya afya mstaafu wa Baraza hilo Dkt. Fredrick Kigadye kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa kanisa katoliki na baraza akiitumikia idara hiyo na majukuu mengine.
Tuzo hiyo 'BENEMERENTI' ilipokelewa kwa furaha na Katibu Mkuu wa TEC Padri Raymond Saba ambaye pamoja na kumpongeza Dkt. Kigadye, amesema watumishi wengine wa baraza lazima waige mfano wa utendaji wake.
Historia ya tuzo hiyo ilianzia miaka ya 1775 enzi za Papa Pius wa VI alipto watunuku tuzo ya Benemerenti wanajeshi waliokuwa wakitetea ukristu enzi hizo na baadaye mwaka 1925 ndipo ikaamuliwa kuwa tuzo hiyo itolewe kwa yeyote atakayekuwa ametoa mchango mkubwa kwa kanisa Katoliki na jamii kwa ujumla kupitia majukumu yake ya kazi za kila siku.



No comments