Ads

Wazazi Wahimizwa kuwa kuwahiza watoto Wapo kupenda masomo ya sayansi.




Mkemia mkuu wa serikali prof Samwel Manyele ,akifanya mahojiano na waandishi wa habari hawapo pichani. (Picha na John Luhende na maktaba ya mwambawahabari)


Na Maria Kaira,Dar 
Mwambawahabari
Wazazi nchini wametakiwa  kuwahimiza vijana wao kupenda masomo ya sayansi ikiwa  na lengo la kuleta chachu katika tasnia hiyo ili taifa liweze kuwa na rasilimali watu.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Michael John katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi na walimu waliofanya vizuri katika masomo ya kemia na baiologia kidato cha nne na cha sita alisema kwa kufanya hivyo kutachangia kuongeza idadi kubwa ya wanasayansi nchini.
John alisema serikali kwa kulitambua hilo wamejipanga kuendeleza na kurithishana ujuzi na ufahamu kwa jamii kutambua sayansi ni masomo kama yalivyokuwa masomo mengine yasitengwe.

“Tufanye jitihada zozote kwa kuhakikisha jamii inatambua umuhimu wa sayansi na mchango wake katika jamii” alisema
Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele alisema anaipongeza hatua iliyochukuliwa na serikali kuimarisha viwango vya elimu  na teknolojia kwa wafanyakazi wa maabara kwa kuwagharamia mafunzo yangazi ndani na nje ya nchi.
“Tulikuwa tunahitaji la kupata mitambo ya kisasa na yenye uwezo wakiteknolojia na uwepowa vifaa vya kutosha na majengo bora ya kufanyiakazi”alisema
Aidha mmoja wa wanafunzi kutoka shule ya sekondari Msolwa Patrick Andrea aliwataka wanafunzi wenzake kupenda masomo ya sayansi na kuachana na dhana ya kuyaogopa masomo hayo.

No comments