Ads

WATANZANIA WASHAURIWA KUJENGA TABIA YA KUFANYA MAZOEZI YA MWILI

 Image result for picha za watu wakifanya mazoezi

WATANZANIA wameshauriwa kufanya  mazoezi kwa wingi  ikiwa na lengo La kupunguza tatizo la magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanayoendelea kukua kwa kasi hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji  wa Impact Afya LMT Bhakti Slah amesema tatizo hilo linaendelea kukua nchini kutokana na asilimia kubwa ya jamii kutofanya mazoezi ipasavyo.

Bhakti amesema Shirikisho la moyo ulimwenguni linaamini kuwa asilimia 60 hadi 85 ya watu ulimwenguni hawafanyi mazoezi ya kutosha hadi kupelekea madhara yatokanayo na tatizo la kutofanya mazoezi.


" Tafiti znaonesha kutofanya mazoezi kunauwezekano mkubwa wa kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza,ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu na kisukari, "amesema

Bhakti amesema uchunguzi wa hivi karibuni umeonesha kuwa idadi ya watanzania wengi hawafanyi mazoezi huku idadi kubwa inayoendelea kuongezeka ni kwaupande wa wasichana kuliko wavulana.

Pia amezishauri jamii kupanga ratiba nzuri ya kufanya mazoezi  ya kutosha na sio bora  mazoezi pamoja na kutumia lishe bora ili kuweza kuepukana na vifo vinavyoendelea kujitokeza .

No comments