WATAKIWA KUWEKEZA KATIKA UONGOZI WA MAISHA NA KUACHA KULALAMIKIA UGUMU WA MAISHA BILA KUCHUKUWA HATUA.
Mwambawahabari
mwambawahabari
Na;John Luhende
Na;John Luhende
Watanzania
wametakiwa kuwekeza katika uongozi
katika shuguli zao ili kuweza kubadilisha maisha yao badala ya kufanya mambo bila kuwa na mwelekeo
wala maengo na kuendelea kulalamikia
serikali kwa ugumu wa maisha ,kwa kuwa serikali haiwezi kumletea mtu fedha
nyumbani kwake,na watu wengi wana ishi maisha magumu na umasikini kwa kuwa
wameshindwa kuongoza .
Hayo
yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa
kampuni ya uchapishaji magazeti ya Global Publisher Eric Shigongo katika
kongamano la uongozi linaloandaliwa na (The Global Leadership
Summit) lililo fanyika jijini Dar es salaam,amesema nivema kila mtu akajitathimini
na kujfahamu ni mambo gani yaliyo changia kumrudisha nyuma kimaendeleo na
kukubaliana na matokeo hayo na kuchukua hatua ya kubadilika na kujipanga upya ,
”kama una
jua ulevi ndiyo ulikurudisha nyuma achana nao,kama ni uvivu,achana nao,kama ni
utegemezi wa fikra uache,kama ni marafiki wabaya wewe badili tabia yako nahao
marafik walikuwa wana kupita kwenda katika mambo yasiyo faa wata ondoka mmoja
mmoja utapata wengine watakao fanana na
tabia yako ya wakatihuo na utakuwa kiongozi
mzuri na utabadilisha maisha yako “ alisema shigongo.
Amesema
jambo lolote katika uongozi bora nialazima likuwe nauongozi ukiharibika kwenye kitu chochote lazima kianguke ,hata
Taifa likikosa uongozi bora lazima lianguke,kitu kikubwa kwa vijana vijana
nilazima uweze kuchoshwa na umasikini na kisha kuchukua hatua wala sikumtupia lawama mtu yeyote .
”kama una
kaa na ndugu yako bila kuwa na manyanyaso nivigumu sana kujiongeza na kuchua
hatua ya kuwa na maisha yako,pia tuache mabo ya kulalamika lalamika kumlaumu Rais kwa maisha magumu ,tuusome
uongozi wake na tuendane na mambo anayotaka tufanye,tukiendelea kupingana naye hatufki mbali maisha yatushinda ” alisema
shigongo.
Mkurugenzi mkazi wa shirka la Global Leadrship Summit Tanzania, bwana Mbuto Mbwayeakizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo ya uongozi( picha na John Luhende) |
Naye mkurugenzi mkazi washirka la Global Leadreshp Summit (GSL) Tanzania bwana Mbuto Chibwaye Amesma wameandaa mafunzo hayo ili viongozi waweze kupata kujifunza mabo mengi ,kwakuwa uongozi sicheo tu bali ni namna unavyoweza kuisaidia jamii na kujisaidia wewe mwenyewe na kuwa na ndoto ya kuwa na maendeleo .
Peter Mayunga Ras mstaafu wa Chuo Cha Elimu ya Biashara CBE , na mjumbe wa kamati ya Global Leader Summit Tanzania ,akizungumza na waandshi wa habari (picha na John Luhende ) |
Post a Comment