Ads

TAASISI YA KANSA OCEAN YAANDAAMATEMBEZI YA HISAN KUCHANGIA MATIBABU NA ELIMU YA SARATANI KWA WANANCHI.



NA. Maria Kaira Dar 
mwambawahabari
Katika kupambana na ugonjwa wa saratani ya matiti nchini Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa kushirikiana  na hospital ya Agha Khan na hotel ya kunduchi beach Octoba 29 watafanya matembezi ya hisani ili kuchangia juhudi za serikali katika kutokomeza saratani ya matiti na kuongeza uelewa kwa jamii.

Lengo la Matembezo hayo nikuchangia ununuzi wa vifaa tiba na kuendesha zoezi la uchunguzi wa saratani,mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Hamis Kingwangalla.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Julius Mwaiselage amesema wamekuwa wanakabiliwa na Changamoto ya wananchi kuwa na dhana potofu yakutoamini kuwa saratani inatibika, wengi wao hufika katika taasisi hiyo ugonjwa ukiwa umeshakomaa.

Mwaiselage amesema taasisi hiyo mwaka 2015/2016 imefanikiwa kuhudumia wagonjwa 33,563, wakiwemo wagonjwa wapya na wale wa marudio 20,297, wanawake 84 walikutwa na saratani ya matiti , ugonjwa huo umeonekana kuwa tatizo kutokana na wananchi waliowengi hufika katika taasisi hiyo wakiwa katika hatua ya mwisho.


"Kwa hapa nchini wagonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi ni wengi zaidi kuliko wagonjwa wa saratani ya matiti ila kuondokana na tatizo hilo serikali imeanza kutekeleza mkakati wa kitaifa wa kuzuia na kudhibiti saratani nchini" amesema
Aidha utekelezaji huo utatekelezwa sambamba na kutoa tiba kwa wale ambao wameshaathirika na ugonjwa huo.

Mwaiselage amesema takwimu zinaonyesha kuwa saratani ya matiti ndio inaongoza duniani kote kwa wanawake kwa kuwa na wagonjwa wapya wapatao milioni 1.7 ambao wanagundulika kila mwaka.

" hapa nchini idadi ya Wagonjwa wapya kila mwaka ni takribani 44,000 lakini wengi wao kwasababu mbalimbali hawafiki hospitali na asilimia 12.5 tu ya wagonjwa ndio wanafika katika taasisi ya saratani ya ocean road kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu na matibabu.

No comments