DC MJEMA:WAMACHINGA TUTAWAPAMAENEO YA KUFANYIA BIASHARAHA ONDOKENI BARABARANI
mwambawahabari
MKUU wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema amewataka Wafanyabiashara ndogo ndogo(Wamachinga) wanaofanya biashara zao katika barabara za mradi wa mabasi yaendayo haraka (Darts) kuondoka mara moja kuanzia wiki ijayo.
Lengo likiwa ni kuwaondolea bughudha wapita njia wanaotumia barabara hizo wakati wa kwenda kukata tiketi zao kwa ajili ya usafiri pamoja na kuziacha njia wazi ili mabasi yapite kwa uharaka.
Agizo hilo amelitoa Dar es Salaam leo wakati wa zoezi la utekelezaji waagizola Rais Dk John Magufuli ya ufanyaji usafi kila ifikapo mwisho wa mwezi.
“Unajua tumekuta wafanyabiashara wanapanga bidhaa zao kwenye vituo vya mabasi wakati wapitanjia na mabasi wanashindwa mahala pakupita na wengine hugongwa na magari”.
Alisema watapelekwa maeneo rasmi watakayoyabainisha rasmi kuanzia wiki ijayo tafauti na hapo atakae kutwa akifanya biashara eneo ambalo sio rasmi sheria itachukua mkondo wake ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Aliongeza kuwa maeneo watakayopewa waende kufanaya biashara zao wateja watawafata na wasiwe wabishi kwani njia za wazi ni za watembea kwa miguu na magari.
Mkuu wa mkoa Dar es Salaam Paul Makonda Oktoba 27 mwaka huu alitoa siku 14 kwa wakuu wa wilaya zote za jiji kuwaondoa wamachinga ambao wamekuwa wakisababisha kero kwa wapita njia huku manispaa ya Ilala ikiwa msitari wa mbele kutekeleza agizo hilo.
Post a Comment