WANAMTANDAO WA MASHIRIKA YANAYOPINGA NDOA ZA UTOTONI WALIA NA MWANASHERI MKUU KUHUSU KUPINGA RUFAA YA KESI YA SHERIA YA NDOA
Na:John Luhende
mwambawahabari
Mtandao wa mashirika yanayopinga ndoa za utotoni nchini umeitaka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kuondoa kusudio la kukata rufaa juu ya kesi ya kupinga ndoa za utotoni iliyotolewa hukumu kuitaka serikali kuondoa baadhi ya vifungu vya sheria ya ndoa ambavyo vinaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri chini ya miaka 18.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mwenyekiti wa mtandao huo ni Valeria Msoka amesema mtandao huo ushitushwa ,kushangazwa na kusikitishwa na taarifa iliyotolewa na mwanasheria mkuu wa serikali kuwa serikali itaka rufaa ili kupinga maamuzi Yaliyojiri tolewa na mahakama kuu kwenye kesi hiyo.
Aidha ameongeza kuwa kitendo cha Mwana sheria mkuu kukata rufaa kina ashiria kuwa serikali INA unaunga mkono ndoa za utotoni jambo ambalo lipo kinyumena mkataba wa kikanda na kimataifa wa kulinda haki na ustawi wa mtoto wa kike ulio sainiwa mwaka 1989 kwa upande wake Koshuma mtegeti ambaye ni mwakilishi wa kulinda utu wa mtoto ameitaja mikoa ya Tabora na Mwanza nimoja ya mikoa inayo ongoza kwa ndoa za utotoni.
Mapema mwezi uliopita mahakama mkuu ya Tanzania ilitoa hukumu dhidi ya kesi ya kupinga vifungu vya sheria vinavyo ruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri chini ya miaka kumi na nane ilyo funguliwa na mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Msichana Initiative dhidi ya mwanasheria mkuu wa Serikali.

Post a Comment