Ads

SERIKALI IMESEMA ITAHAKIKISHA SECTA YA MADINI HAPANCHI INA KUWA SHIRIKISHI





Timothy Marko .

Mwambawahabari

SERIKALI imesema itahakikisha sekta ya uchimbaji wa makaa yamawe na jasi  inakuwa shikirikishi kwa kuwa shirikisha wachimbaji wadogo wadogo nawale wa  kati ilikuweza kukuza sekta ya madini hayo.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada yamkutano ulio wakutanisha wadau hao jijini Dar es salaam Waziri wanishati na madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa ujumuishwaji huo katika uchimbaji wa jasi  na makaa yamawe  kwa wachimbaji wakubwa na wadogo ilikuweza kutatua changamoto baina yao ikiwemo ukosefu wa mitambo .

‘’hii imetokana kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa madini haya katika viwanda vya cement ambavyo hutumia makaa yam awe na madini ya jasi katika uzalishaji wa bidhaa hiyo ilikuweza kukuza soko la madini hayo na kukuza ajira na kupatia serikali mapato kutokana na madini haya ‘’Alisema Waziri Sospeter Muhongo .

Waziri Muhongo alisema kuwa katika ushirikishwaji wa wadau hao wa sekta ya madini hayo utaendana sambamba na ukokotoaji wa kiwango  cha mahitaji ya madini hayo katika viwanda matumizi ya uzalishaji wa bidhaa hiyo .

Alisema kuwa ushirikishwaji katika sekta hiyo ya madini inalenga kukuza misingi yahaki kwa kushilikisha viwanda mbalimbali ikiwemo viwanda vya jasi  na makaa yamawe  kwa kukuza kiwango chautalaamu wa madini hayokatika  ngazi juu .

‘’Tuna tarajia kuwa peleka watalamu wetu hivi karibuni ilikuweza kupata uzoefu namafunzo ya  uchimbaji wa makaa yam awe nchini india na china ‘’Aliongeza waziri Muhongo .

Aidha ,katika hatua nyingine Kamishina kamishina wa kanda ya nyasa ya jumuhia hiyo ya wachimbaji fred Malope amesema jumuia hiyo imekuwa ikikabiliwa nachangamoto ya kuyafikia madini hayo hali inayo changiwa na uhaba wavifaa vya uchimbaji.

No comments