Ilala yashiriki maonyesho ya Nanenane yanayofanyika mkoani Morogoro
Na Jacquiline Mrisho
mwambawahabari
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (kulia) akiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Charles Kuyeko (kushoto) wakihojiwa na mwandishi wa habari katika ufunguzi wa Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) iliyofanyika jana tarehe 01.08.2016 mkoani Morogoro.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando (kulia) wakijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Msongela Palela (kushoto) alipotembelea banda la maonyesho la Manispaa hiyo katika ufunguzi wa Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) iliyofanyika jana tarehe 01.08.2016 mkoani Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (kulia) akiongea na baadhi ya Madiwani wa Manispaa hiyo katika ufunguzi wa Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) iliyofanyika jana tarehe 01.08.2016 mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Msongela Palela (wa pili kushoto) akipata maelezo ya namna ya upandikizaji wa mbegu za samaki kwa njia za kisasa toka kwa Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Msongo Songoro (kulia) katika ufunguzi wa Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) iliyofanyika jana tarehe 01.08.2016 mkoani Morogoro.
Baadhi ya wananchi waliotembelea katika banda la maonyesho la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakipata maelezo ya bidhaa zinazozalishwa na Manispaa hiyo, katika ufunguzi wa Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) iliyofanyika jana tarehe 01.08.2016 mkoani Morogoro.
Post a Comment