Zaidi ya shilingi bilioni 1.6 zinatarajiwa kutumika Katika maboresho ya upatikanaji wa taarifa za wananchi kupitia mfumo wa kieletroniki
Na: John Luhende
mwambawahabari
Zaidi ya shilingi bilioni 1.6 zinatarajiwa kutumika Katika maboresho ya upatikanaji wa taarifa za wananchi kupitia mfumo wa kieletroniki ili kuiwezesha serikali kupanga mipango mbalimbali ikiwemo kutoa huduma za kijamii kwa wananchi.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na katibu mkuu Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe mara baada ya kupokea taarifa ya mfumo wa majaribio kutoka kata ya Mapinga Bagamoyo mkoani Pwani, amesema kuwa mfumo huo utawezesha kupata taarifa katika ngazi ya kaya ,kitongoji na mtaa .
‘’Mfumo huu unaotumia Data base umeweza kutumika katika nchi za Botswana,Syecelles,Tanzania ,Zanzibar na Mauritus na nchi ambazo zina idadi yawatu zaidi milioni 1 ,nchi nyinginezo zinaendelea na juhudi za kuboresha mifumo yake kama Tanzania ‘’alisema Katibu Mkuu Mhandisi Mussa Iyombe .
Aidha mhandisi Iyombe amesema kuwa mfumo huo utawezesha kupunguza gharama na mzigo mkubwa kwa serikali ambapo sensa ya watu na makazi inayofanyika baada ya miaka kumi hutumia fedha nyingi ukilinganisha na mfumo huu,na pia utasaidia kupunguza udanganyifu na uhalifu nchinikwakuwa kila mtu atakuwa ameandikishwa katika mfumo huu na hataweza kudangaya,
alisema Mfumo huo umewahi kutumika katika nchi za ulaya Sweden Norway nanchi Nyinginezo katika ukanda wa bara la ulaya na amerika .
‘’Mfumo huu sio jambo jipya kwa nchi yetu tulikuwa na mfumo huu ambao tulikuwa tunatumia dafutari maalumu la ukaazi kinacho fanyika hivi sasa nimaboresho yataarifa kwa njia ya mfumo wa kiletroniki ‘’Aliongeza Katibu Mkuu Mussa Iyombe .
Naye diwani wa kata ya Mapinga wilayani bagamoyo ambako mfumo huu umeanza kwa majaribio amesema mfumohuu umepunguza kwa kiasi kikubwa udanga nyifu wa nyaraka na kupotea kwa kumbu kumbu ambapo awali wali hifadhi katika madaftari na sasa wananchi wanaweza kusajili vizazi na vifo bila usumbufu na walimu umewasaidia kubaini wanafunzi wanaoanza shule darasa la kwanza kila mwaka.
Post a Comment