 |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akiwasili katika Ofisi ya British Council Tanzania kwa ajili ya kuzindua Fursa ya Sanaa
inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11 Julai, 2016 Jijini Dar es Salaam.Kulia ni mwenyejji wake ambaye ni Kaimu Mkurugenzi British Council Tanzania, Bi. Nesia Mahenge.
|
 |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwahutubia wageni waalikwa pamoja na wanahabari kabla ya kuzindua Fursa ya Sanaa
inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11 Julai, 2016 Jijini Dar es Salaam.
|
 |
Kaimu Mkurugenzi British Council Tanzania, Bi. Nesia Mahenge akiwahutubia wageni waalikwa pamoja na wanahabari wakati wa Uzinduzi wa Fursa ya Sanaa
inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11 Julai, 2016 Jijini Dar es Salaam. |
 |
Msanii wa kike toka Taasisi ya Culture and Development East Africa, Bi. Zuhura Seng'enge akiwapa burudani ya shairi wageni waalikwa pamoja na wanahabari wakati wa Uzinduzi wa Fursa ya Sanaa
inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11 Julai, 2016 Jijini Dar es Salaam. |
 |
Wasanii Gwakisa Mwambungu (kushoto) pamoja na Khalila Mbowe wakiwapa burudani ya nyimbo wageni waalikwa pamoja na wanahabari wakati wa Uzinduzi wa Fursa ya Sanaa
inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11 Julai, 2016 Jijini Dar es Salaam. |
 |
Mkuu wa Masuala ya Sanaa Kenya na Afrika Mashariki toka
British Council, Bi. Rocca Gutteridge akiwahutubia wageni waalikwa pamoja na wanahabari wakati wa Uzindua wa Fursa ya Sanaa
inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11 Julai, 2016 Jijini Dar es Salaam. |
 |
Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Bi. Leah Kihimbi akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa ajjili ya kutoa hotuba kwa wageni waalikwa kabla ya kufanyika kwa Uzinduzi wa Fursa ya Sanaa
inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11 Julai, 2016 Jijini Dar es Salaam. |
 |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto)
akizindua Fursa ya Sanaa inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11
Julai, 2016. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Bi. Leah
Kihimbi, wa pili kulia ni Mkuu wa
Masuala ya Sanaa Kenya na Afrika Mashariki toka British Council, Bi. Rocca
Gutteridge na wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi British Council Tanzania, Bi.
Nesia Mahenge.
|
 |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kushoto)
akiangalia bango lenye ujumbe kuhusu fursa ya sanaa
inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11 Julai, 2016. Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Bi. Leah Kihimbi, wa pili kulia ni Mkuu wa Masuala ya Sanaa Kenya na Afrika
Mashariki toka British Council, Bi. Rocca Gutteridge na wa pili kushoto ni
Kaimu Mkurugenzi British Council Tanzania, Bi. Nesia Mahenge.
|
 |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiimba
huku akipiga gitaa mara baada ya kuzindua Fursa ya Sanaa
inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11 Julai, 2016 Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi British Council Tanzania, Bi. Nesia Mahenge.
|
 |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye
akiwaonyesha Wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)
picha aliyochorwa na mmoja wa Wasanii mara baada ya kuzindua Fursa ya Sanaa inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11 Julai, 2016 Jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi British Council Tanzania, Bi. Nesia Mahenge.
|
 |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye
(aliyevaa suti ya Kaunda) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa British Council Tanzania pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara mara baada ya Uzinduzi wa Fursa ya Sanaa inayodhaminiwa na British Council Tanzania 11 Julai, 2016 Jijini
Dar es Salaam.
|
(Picha/Stori na Benedict Liwenga)
WASANII
nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya kazi za sanaa ambayo inadhaminiwa na
British Council Tanzania.
Wito
huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati wa Uzinduzi wa Fursa ya Sanaa kwa Tanzania na
Afrika Mashariki ambayo Mdhamini wake ni British Council Tanzania.
Mhe.
Nnauye amesema kuwa, uzinduzi wa fursa hiyo utawasaidia wasanii nchini, Mashirika
mbalimbali yakiwemo Makampuni ya ndani ya Tanzania pamoja na Afrika Mashariki pamoja
na Uingereza.
Amesema
kuwa, fursa hiyo ni kubwa kwa wasanii nchini na kwa Taifa kwa ujumla, hivyo
ameipongeza British Council Tanzania kwa kuja na wazo hilo zuri kwa manufaa ya
wasanii nchini.
‘’Napenda
nichukue nafasi hii kuwapongeza British Council Tanzania kwa kuwashirikisha
wasanii na Makampuni mbalimbali na kuhakikisha kuwa fursa hizi zinamfikia kila
msanii ndani ya Tanzania na kuwawezesha kushirikiana pamoja kwenye Sekta ya
Sanaa na Utamaduni ndani ya Afrika Mashariki na Uingereza kwa ujumla’’,
alisema, Mhe. Nnauye.
Ameongeza
kuwa Serikali kupitia Wizara yake imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali
ndani na nje ya Tanzania katika kuwawezesha wasanii katika kukuza vipaji
vyao na kupata fursa zinazowawezesha
kuitangaza nchi yao.
‘’Serikali
inatambua changamoto zinazowakabili wasanii wetu na imejikita katika
kuhakikisha kuwa inatoa fursa zilizopo
kwa wasanii wetu’’.
Mhe.
Nnauye amesema kuwa, Serikali itaendelea kuwa mstari wa mbele kuhakikisha
kwamba inazidi kushirikiana na British Council Tanzania na wadau mbalimbali ili
kukuza vipaji vya wasanii hao.
Kwa
upande wake Mkuu wa Masuala ya Sanaa Kenya na Afrika Mashariki toka British
Council, Bi. Rocca Gutteridge amesema kwamba, fursa inayodhaminiwa na British
Council inalenga kuwawezesha Wasanii wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla
kuwa karibu kwa kushirikiana katika vipaji vyao na hivyo wameanzisha na
platfomu maalum ambayo wasanii hao watakuwa wakisaidiana katika kazi zao.
Naye
Kaimu Mkurugenzi British Council Tanzania, Bi. Nesia Mahenge amesema kuwa katika
kuanzishwa wa fursa hiyo, kutakuwa na Miradi kati ya mitatu hadi tano ambayo
itachaguliwa katika mwaka wa 2016/17
ambapo kila mradi utapewa fedha kiasi cha Euro elfu 20.
Ameongeza
kuwa, British Council inalenga kusaidia zaidi ya wasanii 60 wa Afrika Mashariki
ambapo wataweza kusafiri ndani ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha miezi tisa ijayo.
Post a Comment