Vijana waaswa kujiajiri kupitia filamu.
Na Shamimu Nyaki WHUSM.
mwambawahabariblog
Serikali imewaasa Vijana nchini kujiajiri kupitia filamu kwakua ni Sekta ambayo inatoa nafasi kubwa kwa kundi hilo lenye uhitaji mkubwa wa ajira hapa nchini.
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo alipokuwa akitoa mafunzo kwa Vijana kuhusu Umuhimu wa Sekta ya Filamu katika kutoa ajira kwa vijana.
Amesema kuwa Sekta ya Filamu ni Sekta ambayo inaweza kusaidia vijana kujiajiri kwa kuwa ina vipengele vingi vinavyoweza kuwasaidia ikiwemo uandishi wa Mswaada, utengenezaji wa Filamu, uigizaji, upigaji picha na kuhariri.
“Takribani asilimia 70% ya watu wamepata ajira kupitia filamu hivyo ni vyema na nyie mkatumia elimu mnayopata hapa na vipaji vyenu kufanya filamu ili kujikomboa kiuchumi”Alisema Bi Joyce.
Ameongeza kuwa ni vyema Vijana kuwa wazalendo kwa kutengeneza Filamu ambazo zitakuwa na maadili ya kitanzania ambazo zitakuwa zinatazamwa na kila mtu bila kujali umri kwakua Filamu mbali ya kuelimisha pia inatoa burudani.
Aidha Kijana Hafidh Omary ameishukuru Bodi ya Filamu kwa elimu iliyotoa kwa vijana hao ambapo wameweza kujua mambo mengi kuhusu Filamu ikiwemo hatua gani za kufuata kabla ya kutengeneza Filamu ili kuepuka kutoa filamu ambayo haiwezi kupata kibali kutoka Bodi ya Filamu.
“Binafsi namshukuru Katibu Mtendaji kuanzia sasa najua kuwa kabla ya kufanya filamu lazima kwanza niende Bodi ya Filamu nikapewe kibali na baada ya kutengeneza filamu yangu niirudishe tena katika ofisi hizo ili ikakaguliwe niweze kutoa Filamu bora na yenye Madili”. Alisema Bw Hafidh.
Hata hivyo Bodi ya Filamu ina lengo la kuwasadia vijana kujifunza zaidi ambapo inatarajia kuwapeleka watu thelathini nchini Nigeria kujifunza zaidi filamu ili kuinua soko la hapa nchini kwa wasanii wa filamu.
Post a Comment