NAIBU WAZIRI WA AFYA DK. HAMISI KIGWANGALLA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA VIONGOZI WA MFUKO WA ABBOTT (ABBOTT FUND) KUTOKA MAREKANI.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto)
akizungumza na viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund)
kutoka nchini Marekani na wale wa Tanzania waliomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam kuzungumza naye kuhusu masuala mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za Afya na Elimu kupitia
program mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo nchini. Kutoka Kulia ni Makamu
Mtendaji wa Rais wa Mfuko wa Abbott, Stephen Fussell na Makamu wa Rais Mwandamizi
wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund Bi.Elaine Leavenworth (katikati).
Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund)
Bi.Elaine Leavenworth (kulia) akimweleza Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) juu ya namna Mfuko wa Abbott
ulivyojipanga kuendelea kutekeleza Program mbalimbali nchini Tanzania zikiwemo
za Matumizi ya Teknolojia ya kisasa katika utoaji wa Tiba, maabara za kisasa,
dawa na vifaa vya mafunzo kwa wanafunzi wa masomo ya Sayansi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto)
akifurahia jambo na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund) Bi.Elaine
Leavenworth (kushoto) mara baada ya ujumbe wa viongozi wa mfuko huo kutoka nchini
Marekani kumtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Ujumbe wa viongozi
wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund) kutoka Marekani ukimsikiliza Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake
leo jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Mfuko wa Abbott (Abbot Fund) nchini Tanzania
Andy Wilson akielezea utayari wa Mfuko huo katika kuzitafutia ufumbuzi
changamoto zinazoikabili sekta ya Afya na Elimu nchini kupitia ufadhili wa Programu
mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo kwa niaba ya Watu wa Marekani. Picha/ Aron Msigwa .
Post a Comment