Ads

KITUO CHA UWEKEZAJI NCHI (TIC)KUFANYA MAKUBWA ZIARA YA WAZIRI MKUU WA INDIA

 Mwambawahabari

Meneja uhusiano wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Daudi Riganda (kulia) akizungumza na waandishi wahabari (hawapo pichani) katika  ukumbi wa habari Maelezo jijini Dar es salaam , aliyepo Julia ni Zacharia Kingu mratibu wa idara ya uhamasishaji uwelezaji wa TIC.(picha zote na John Luhende)

Na:John Luhende

 mwambawahabariblog

Kituo cha Uwekezaji  Tanzania (TIC) Kwa kushirikiana na na Taasisi ya Sekta binafsi Tanzania (TPSF) pamoja na Shirikisho la Biashara la Viwanda la India (FICCI) kwapamoja wameandaa kongamano la Uwekezaji litakalofanyika Julai 10 mwakahuu ,ambapo Kongamano hilo limelemga katika kuwaleta pamoja wafanyabiashara wa nchi hizi mbili ili kubadilishana uzoefu katika masuala ya biashara na Uwekezaji.

Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam Meneja uhusiano kituo cha Uwekezaji Daudi Riganda amesema kuwa Kongamano hilo limekuja kufuatia tukio la ujio wa Waziri Mkuu wa India Mahinra,  Mod ,ambapo itahusisha wafanyabiashara kutoka sekta za Kilimo, Viwanda, Miundombinu, Elimu, Afya, Nishati na Maji.

Aidha Riganda ameongeza kuwa kulingana na takwimu za kituo cha uwekezaji kati ya mwaka 1990 na Juni 2016, kituo kimeweza kusajili jumla ya miradi 442 ya Kimarekani kutoka India yenye thamani ya Dola za Kimarekani Billioni 2.122.



Pamoja na hayo bwana Riganda amewakaribisha wawekezaji wandani kuhudhuria kongano hilo litalalo fanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro ulioko katika bank mkuu ya Tanzania (BOT) kuanzia saa 3:00 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki.

No comments