Ads

BARAZA LA WAGANGA WA TIBA ,NA USHAURI NA UTAFITI WA DAWA ASILI TANZANIA ( BAWATA ) LAPINGA KUFUNGIWA KWA WENZAO





Na: John Luhende  
mwambawahabariblog
Baraza la waganga wa tiba,ushauri na utafiti wa  dawa asilia  Tanzania  (BAWATA) limesema lime sikitishwa na  na utendaji wa  kazi  unaofanywa na  Baraza la tiba  Asili na tiba mbadala   kwa kuvifungia vituo vya   Fore plan  Dr Mwaka ‘  The father gate  sanitarium clinic, naMandai  Heabal clinic  kwa makossa yasiyo kuwa ya msingi .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam  mwenyekiti wa chama hicho Dr Mohamed Matokeo  amesema kuwa  kuvifungia vituo hivyo  ni uonevu kwa ni wahusika hawakuhojiwa    na kutengeneza mgogoro usio wa msingi baina  ya chama hicho na  chombo  hicho cha  serikali , ameongeza kuwa kufungwa kwa vituo hivyo ni kutokana na mgongano wa kima slahi  ambao umeonekana wazi wazi  kuwa wenye vituo hivyo wa pata wateja wengi .

Aidha amemwomba Rais  wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli  kulitupia  macho Baraza  na Wizara  mama  ili kujua hali halisi , na ameomba Baraza  kurudishwa katika Wizara ya  Elimu   kuliko kuwa  Wizara  ya Afya,  na wameomba  sheria za usjili wa waganga  ziangaliwe upya  kwani kuna waganga  kwani kuna mambo yana yo  kwamisha waganga  wasisajiliwe na kujenga  mazingira ya Rushwa  hasa kwa watendaji wa kata ,vitongoji na vijiji .

,,Tuna patwa na wasiwasi  sana kuona  juhudi za Waziri  wa Afya  zinaweza kukwamishwa na watendaji  wa Baraza pamoja  na Wizara ya Afya ,,


Ameongeza kuwa hatua hii  ya kufunga vituo hivyo itaathili waTanzania wengi walio kuwa wkipata huduma   za kimatibabu katika vituo hivyo  pia ajira za watu wengi ambao wali kuwa  wakihudumia zitakuwa mashakani  hivyo ni bora inge angaliwa njia nyingine bora ya badala ya njia hii ilyo tumika 

No comments