RICHARD QUEST WA CNN AFURAHISHWA NA VIVUTIO VYA UTALII TANZANIA KATIKA MAONYESHO YA INDABA
MWAMBAWAHABARIBLOG
Kwa mara nyingine tena Tanzania inashiriki katika onesho la kimataifa la Utalii la INDABA yanayofanyika huko Afrika Kusini maonesho hayo yalianza jana tarehe 7 Mei na yanatarajiwa kumalizika tarehe 9 Mei, 2016. jijini Durdan, Bodi ya Utalii (TTB) ndio waratibu wa onesho kwa upande wa Tanzania. Katika onesho hili TTB inashirki pamoja na taasisi za TANAPA na Mamlaka na Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na makampuni mbalimbali binafsi Zaidi ya 30 ya sekta ya Utalii .
Katika siku yake ya kwanza Banda la Tanzania limetembelewa na wadau wengi wakiwemo watalii, waandishi wa habari za utalii, mawakala wa Utalii nk. Miongoni mwa watu mashuhuri waliotembelea Banda la Tanzania ni Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest ambaye alifurahishwa na vivutio vua utalii nchini Tanzania mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Maofisa wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB.




Post a Comment