Mkurugenzi Mtendaaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu Nchini Tanzania LHRC Bi HELLEN KIJO BISIMBA akizungumza na wanahabari habari hawapo pichani
mwambawahabariblog
Na :John Luhende
Kwa siku za hivi karibuni Tasnia ya Habari imeanzakuingiliwa na baadhi ya watumakanjanja wasio naujuzi kwa kurekodi baadhi ya matukio ya kidhalilishaji hasa wa kijinsia kupitia simu za mkononi pasipo kujua athari zake kwa jamii.
Kwa kutambua hilo mashirika yanayo tetea hakiza binadamu na Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)yame toa tamko na kulaan vitendo hivyo kwa watumiaji wa Mitandao ya Kijamii kutuma nakusambaza picha zisizo na maadili na kuzingatia utu wa mtu
Akitoa tamko hilo mbele ya Wanahabari Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dk. Hellen Kijo – Bisimba ameitaka serikali kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wanaotumia vibaya mitandao hiyo bila kujali hadhi yao kwa jamii.
“Tunaitaka serikali iwachukulie hatua kali za kisheria kama ambavyo tumeona hatua zikichukuliwa kwa waliomdhalilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”. Amesema Bisimba
Pamoja na hayo Dr Kijo ametoa wito kwa jamii kutosambaza picha zinazodhalilisha utu wa binadamu katika matukio mbalimbali ikiwemo matukio ya ukatili wa majumbani, ukatili wa kijinsia, ukatili kwa watoto, ajali za barabarani na vifo kwakuwa kufanya hivyo nikukiuka haki za binadamu.
Post a Comment