GLOBAL PEACE FOUNDATION YAWATAKA VIJANA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA KUDUMISHA AMANI
Shirika la Global Peace Foundation Tanzania limewataka vijana wa kitananzania kutumia vizuri mitandao ya kijamii katika kudumisha na kulinda amani ya taifa, ambayo ni tunu kubwa ya taifa la tanzania na endapo itatoweka ni kazi kubwa kuirejesha.
Hayo yalizungumzwa na kiongozi mkuu wa Global peace Foundation Martha Ng’ambi wakati wa warsha ambao iliandaliwa katika chuo kikuu cha Dar es salaam katika kitivo cha habari, ambapo amewataka wana habari kushiriki katika zooezi zima la kuilinda amani nchini hasa kwa kutumia taaluma yao.
Taasisi hiyo ilizungumza kwa njia ya mdahalo na wanafunzi katika chuo kikuu dar es salaam ambao wanasoma masomo ya waandishi wa habari na kuweza kuibua changamoto nyingi na nini kifanyike ili vijana waweze kupambana na masuala ya uvunjifu wa Amani katika tasnia ya habari.
Mmoja kati ya wanafunzi hao munira Hussein alisema kuwa waandishi wa habari wana nafasi kubwa katika kulinda Amani, huku akitolea mfano mauji ya kimbali ambayo yalifanyika nchini Rwanda mwaka 1994 kuwa yalichangiwa na vyombo vya habari. “Sisi waandishi tunaweza kuifanya jamii ya watu kuwa na maono mazuri kama tutatumia kalamu zetu vizuri”.
Kwa upande wake moja ya wageni rasmi alikuwapo Anthony Luvanda ambaye ni mwanaharakati na amewataka vijana wa kitanzania ambao wako katika tasnia ya habari kuifanya kisasa kwa kuweka vitu chanya na kuongeza kuwa mtu ambaye anataka kusomea uandishi wa habari basi awe na moyo na msukumo wa kuisomea kwani mwandishi wa hjabari mwenye wito wake atafanya kwa moyo wake woto, na watu makini ufuta maono yao.
Shirika la Global peace foundation limekuwa likijitokeza mara kwa mara katika kupigania Amani kwa watanzania, kwa kuandaa warsha mikutano mbalimbali katika kuhakikisha nchi inakuwa ya Amani na utulivu.
Post a Comment