RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWAAPISHA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA 10 LEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.
mwambawahabariblog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Jumanne Abdallah Sagini
(kulia) kuwa Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Simiyu leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Simiyu
akisaini Hati ya kiapo chake mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Selestine Muhochi
Gesimba kuwa Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Geita leo Ikulu jijini Dar es
salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Dkt. Thea Medard Ntara kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Mhandisi Zena Said kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Hati ya Kiapo cha Katibu Tawala
mpya wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said mara baada ya kumwapisha leo Ikulu jijini
Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Albert Gabriel Msovela kuwa Katibu
Tawala mpya wa mkoa wa Shinyanga leo Ikulu jijini Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendendea kazi Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Shinyanga Bw.
Albert Gabriel Msovela mara baada ya kumwapisha, Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Dkt. Angelina Mageni Lutambi
kuwa Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Singida leo, Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na Makatibu Tawala wa mikoa 10 walioapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Wengine pamoja nae ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) na
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi, Balozi John William Kijazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John William Kijazi wakiwa katika
picha ya pamoja na waandishi wa Habari waliohudhuria hafla fupi ya kuapishwa
kwa Makatibu Tawala wa Mikoa 10 Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Makatibu Tawala wa Mikoa wakiapa mara
baada ya kujaza Fomu za maadili kwa viongozi wa umma zinazowataka kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu
za Utumishi wa Umma, Ikulu jijini Dar es salaam.
Makatibu Tawala wa Mikoa wakijaza Fomu
za maadili ya Viongozi wa Umma zinazowataka kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu
za Utumishi wa Umma, mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi
John William Kijazi akizungumza na Makatibu Tawala wa Mikoa mara baada ya
kujaza Fomu za maadili ya Viongozi wa Umma, Ikulu jijini Dar es salaam.
Na. Waandishi Wetu - Dar es salaam.
Na. Waandishi Wetu - Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amewaapisha Makatibu Tawala wapya
wa mikoa 10 aliowateua Aprili 25 mwaka huu katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu
jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John
William Kijazi.
Makatibu Tawala walioapishwa
leo ni Bw. Jumanne Abdallah Sagini ambaye
anakwenda kuwa Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Selestine Muhochi Gesimba Katibu
Tawala mpya wa mkoa wa Geita na Dkt. Thea Medard Ntara Katibu Tawala mpya wa
Mkoa wa Tabora.
Wengine ni Mhandisi Zena Said ambaye anakwenda kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bw. Albert Gabriel Msovela Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Shinyanga, Dkt.
Angelina Mageni Lutambi aliyeapishwa kuwa Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Singida,
na Dkt. Angelina Mageni Lutambi ambaye anakwenda kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Singida.
Pia amewaapisha Bw.
Richard Kwitega kuwa Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Arusha, Bw. Armatius C. Msole kuwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kagera, Mhandisi Aisha Amour ameapishwa kuwa Katibu Tawala wa
mkoa wa Kilimanjaro na Bw. Zubeir Mhina Samataba aliyeapishwa kuwa Katibu
Tawala wa mkoa wa Pwani.
Mara baada kuapishwa
Makatibu Tawala hao wamejaza fomu za Maadili kwa viongozi wa umma zinazowataka wazingatie Sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia
Utumishi wa Umma.
Akizungumza na
Makatibu Tawala hao mara baada ya kukamilisha zoezi la ujazaji wa fomu hizo Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John William Kijazi amewataka wazingatie maadili
na mipaka yao ya kazi na kuepuka kuwabagua watumishi wanaowaongoza.
Balozi Kijazi amewataka
waishi kwa kufuata miiko na maadili kwa viongozi wa umma yaliyoanishwa kwenye
fomu walizojaza ili kuepusha mgongano wa kazi na maslahi mahali pa kazi.
Amewaagiza Makatibu
Tawala hao kuwasimamia watumishi walio
chini yao ili maadili waliyokubali kuyazingatia yafuatwe na watumishi walio
chini yao.
“Napenda kuwajulisha
kuwa tuko kwenye awamu nyingine, na
mnajua kuwa awamu hii ikisema jambo maana yake litekelezwe, msije mkaliacha
mezani na kuendelea na mambo mengine” Amesisitiza Balozi Kijazi.
Amewataka Makatibu
Tawala hao kushirikiana kikamilifu na watumishi wanaowaongoza ili waweze
kutatua kero mbalimbali za wananchi kwa kuyashughulikia kwanza matatizo watakayoyakuta katika vituo
vyao kabla ya kuanzisha mambo mapya.
Kwa Upande wao
Makatibu Tawala walioapishwa wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wamejipanga
kikamilifu kutekeleza kwa vitendo Kauli
mbiu ya “Hapa Kazi Tu” kwa kuwatumikia wananchi katika maeneo waliyopangiwa.
Bw.
Zubeir
Mhina Samataba aliyeapishwa kuwa Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Pwani amesema
kuwa katika uongozi wake atahakikisha kuwa anashirikiana na watumishi wenzake kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa mkoa wa Pwani.
Amesema kuwa ataweka
mkazo katika kuwahamasisha wananchi kufanya kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo
ya kiuchumi, kukuza sekta ya kilimo cha mazao ya Chakula, Biashara na Elimu mkoani
Pwani.
Aidha,amesisitiza kuwa anakwenda kulisimamia kikamilifu suala la uhakiki wa
Watumishi hewa katika mkoa wake pamoja
na kushughulikia migogoro ya ardhi iliyo katika mkoa wa Pwani.
Naye Dkt. Angelina
Mageni Lutambi ambaye aliyeapishwa kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Singida
akizungumza mara baada ya kuapishwa amesema kuwa jukumu lililo mbele yake ni
kuhimiza uchapakazi miogoni mwa watumishi wa mkoa wa Singida.
“Nimelipokea jukumu
hili nililokabidhiwa na Mhe. Rais kwa Moyo wa dhati, nitahakikisha kuwa
ninawatumikia wananchi na kuwahimiza
viongozi wenzangu kutimiza wajibu wao ipasavyo” Amesisitiza Dkt. Angelina
Lutambi.
u wao ipasavyo” Amesisitiza Dkt. Angelina
Lutambi.
Post a Comment