Wakati zikishuhudiwa taasisi za njani na nje ya nchi pamoja na baadhi ya Watanzania wakitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli kulingana na utendaji wake, lakini kwa Vyama vya Upinzani mambo yamekuwa tofauti kwa madai kuwa hawaridhishwi na utumbuaji majipu wake kwa baadhi ya viongozi wa Umma.
Hatua hiyo imefuata baada ya kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe kwa kile kilichodaiwa kufanya ubadhirifu wa mali za Umma kwa kuisababishia serikali hasara ya takribani shilingi billioni tatu.
Kwa mujibu wa ripoti ya Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Dar es Salaam Henry Kilewo imesema kuwa mfumo anaotumia Rais Magufuli katika kupambana na ubadhirifu wa mali za Umma kwa kutumbua majipu ni ya ubadilishaji wa uongozi kutoka ule ulioachwa na sasa umerejeshwa upya, huku ripoti hiyo ikimtaja Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuwa naye anafanya vitu vinavyoleta sintofahamu kama kweli yupo kwa maslahi wa wananchi au Chama.
“Mhe Rais anachokifanya ni kiini macho kwa wananchi kwani anatumbua na kuwabakiza wengine, kwani inajulikana Mkurugenzi hawezi kusaini pesa bila sahihi ya Meya wake na kamati za Fedha hivyo kwa vyovyote vile Masaburi anahusika kwanini Mkurugenzi afukuzwe kwa haraka vile au kisa kaongea Makonda?”.Alihoji Kilewo
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Dar es Salaam Bernard Mwakyembe amesema kuwa wanaliandikia barua ya onyo Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kutokana kile alichodai kwamba wameegamia chama tawala pekee.
Post a Comment