KUBENEA AHUKUMIWA KIKIFUNGO CHA NJE MIEZI MITATU
Na.
Raymond Mushumbusi
mwambawahabariblog
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saeed Kubenea
kifungo cha nje cha miezi mitatu kutokana kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi
ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ambaye sasa ni Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam.
Akisoma hukumu hiyo leo Jijini Dar es Salaam Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Thomas Simba amesema kuwa mahakama imeamua kumpa mshitakiwa adhabu ya kifungo hicho kwa kuwa ndilo kosa lake la kwanza, hivyo Mshatakiwa anastahili kupata adhabu ya huruma.
Chini
ya adhabu hiyo iliyotolewa chini ya kifungu no 89 kifungo kidogo cha kwanza
Mhe. Kubenea hatakiwi kufanya kosa la aina yoyote ambalo litamsababisha
arudishwe tena mahakamani na endapo itatokea akafanya hivyo mahakama itampa
adhabu ya kifungo cha kwenda jela.
Awali
kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo mshtakiwa Said Kubenea mbele ya Hakimu
Mkazi Thomas Simba alipewa nafasi ya kujitetea ni kwanini asipewe adhabu
kali kwa kosa alilolitenda ambapo alieleza Mahakama hiyo kuwa hakuwa na nia
mbaya ya kwenda kufanya fujo eneo la tukio ambapo kulikuwa na mgomo wa
wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha TOOKU cha jijini Dar es salaam bali
alikwenda kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgomo huo akiwa kama mwakilishi wa
wananchi wa jimbo la Ubungo.
Ikumbukwe
kuwa Jalada la kesi hiyo na 320 ya mwaka lilifunguliwa na Jamhuri dhidi ya Said
Kubenea kwa kosa la kutumia lugha ya matusi kwa aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni Paul Makonda, Aidha upande wa washtakiwa wameonyesha kutoridhishwa na
hukumu hiyo na wameomba kukata rufaa.
a
Post a Comment