KATIBU CHAMA CHA WALIMU (CWT)MKOA WA DAR ES SALAAM AZUNGUMZA NA MWAMBAWAHABARI NA AMPONGEZA JPM ,NA KUTOA YAMOYONI KUHUSU CHANGAMOTO ZA WALIMU ( MSIKILIZE HAPO CHINI AUDIO)
mwambawahabariblog
Chama cha walimu mkoa wa Dar es salaam CWT kimeipongeza serikali ya awamu ya tano baada ya kuonyesha juhudi mbalimbali za kutatua kero za walimu ikiwemo kuanza kuwalipa malimbikizo ya madai yao.
Akizungumza na mwambawahabari, jijini Dar es salaam katibu mkuu wa chama cha walimu mkoa wa
Dar es salaam Bwa Abdallah Mkaula amesema jitihada hizo za serikali ya awamu ya
tano zitaweza kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu na
kurudisha nia ya kujituma zaidi.
Aidha ameongeza kuwa mbali na kuwepo kwa jitihada za kupunguza
madai ya walimu bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya
kutopashindwa madaraja kwa wakati na kutolipwa mapema fedha ya kujikimu
.
Post a Comment