ASILIMIA 71 YA WATANZANIA HAWATAKI KUFANYA KAZI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Jenista Mhagama,akizindua
ripoti ya matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014
katika Viwanja vya Karimjee,Dar es Salaam, . Wengine wanaoshuhudia ni kushoto
kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu nchini,Dk.Albina Chuwa, Mkurugenzi wa Sensa
ya watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo na Mwakilishi kutoka Shirika la
Kazi Duniani,Marry Kawar.
Na Raymond Mushumbusi
mwambawahabariblog
Utafiti uliofanyika hivi karibuni na Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS) umebaini kwamba asilimia 71 ya watanzania wanatumia muda
mwingi kufanya shughuli zisizokuwa za uzalishaji mali wala tija binafsi kwao na
Taifa kwa ujumla
Akizundua taarifa ya utafiti huo leo jijini
Dar es salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Ajira,Vijana
na watu wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa idadi hiyo
hufanya kazi zisizoleta tija kwao na taifa na muda mwingi huutumia kujihudumia
binafsi kwa kulala na starehe nyingine.
Ameeleza kuwa takwimu hizo zinaonesha wazi ni
kwa namna gani watanzania wanashindwa kujishughulisha katika kufanya kazi zenye
kuwaingizia kipato na badala yake wanatumia muda wao mwingi kufanya shughuli zisizo
za uzalishaji hasa kufanya starehe mbalimbali.
“ Ndugu zangu watanzania unakuta mtu
amekaa baa au anacheza “poll table” kuanzia asubuhi mpaka jioni na hujui
anafanya kazi gani ya uzalishaji, ndugu zangu tuone aibu basi tujishugulishe
tulijenge taifa letu ili kujiletea maendeleo yetu na nchi yetu.”
Aidha, matokeo hayo yamebainisha kuwa asilimia
18.5 ya wananchi wanafanya kazi za uzalishaji na asilimia 10.6 ni wale
wanaofanya shughuli za nyumbani zisizo na malipo huku uchambuzi wa kijinsia
ukionesha kuwa wanaume asilimia 23.8, wanatumia muda mwingi kwenye shughuli za
kiuchumi ikilinganishwa na asilimia 13.5 ya wanawake.
Amefafanua kuwa wanawake ambao ni asilimia
16.5 katika utafiti huo wanatumia muda mwingi kufanya kazi za nyumbani zisizo
na malipo ikilinganishwa na asilimia 4.4 ya wanaume.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisa ya
Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa upatikanaji wa Takwimu
hizo utaisaidia Serikali kupata mbinu sahihi za kuondokana na tatizo la ajira
nchini kwa kuunganisha nguvu kutoka sekta isiyo rasmi ili kuleta changamoto
katika soko la ajira nchini.
Amesema kuwa hii ni mara ya tano Tanzania
inafanya utafiti huo na kubainisha kuwa ulianza mwezi Januari hadi
Desemba, 2015 ukitumia sampuli ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka
2012 iliyotumika kupata taarifa sahihi ya takwimu hizo.
Aidha, amebainisha kuwa ili kufanikisha
utafiti huo NBS imeshirikiana na wadau mbalimbali ikwemo Wizara ya kazi na
Ajira,Shirika la Kazi Duniani (ILO),Benki ya Dunia (WB),Benki ya Maendeleo ya
Afrika(ADB) na Asasi zisizo za Kiseikali.
Post a Comment