Umoja wa Waliosoma Kigoma Sekondari mwaka 1991 -1994 wazinduliwa
mwambawahabari
Na: Mwandishi Wetu.
mwambawahabari
Umoja wa waliosoma shule ya sekondariKigoma mwaka 1991-1994 umezinduliwa leo rasmi baada ya mwanasheria wao Wakili
Marko Anthony Nsimba kukabidhi cheti cha kusajiliwa na katiba ya umoja huo kwa
wanaumoja huo hii leo.
Akizungumza baada ya kupokea cheti hicho,
Mwenyekiti wa Umoja huo kwa niaba ya wanachama Dk Nelson Boniface amesema,
lengo kuu la UWKS kuwakutanisha pamoja wanafunzi waliosoma Shule hiyo kuanzia
1991-94.
Boniface ameongeza kuwa pamoja na
kukutana, lakini pia nikusaidiana katika shida na raha kushiriki katika mambo
mbalimbali ya maendeleo katika taifa letu sambamba na kutoa ushauri, michango
ya misaada ya hali na mali kwa jamii yenye uhitaji.
Aidha umoja utashirikiana na taasisi
mbalimbali za Kiserikali na zisizo za Kiserikali katika maendeleo ya jamii ya
watanzania.
Wakati huohuo amezitaja baadhi ya
changamoto ambazo umoja huo umekutana nazo ikiwa ni pamoja na baadhi wahitimu
wenzao kutoamini kuwa wanaweza kuwa na umoja na wengine wakithubutu kusema ni
kupoteza muda.
“pamoja na kupotezana kwa Zaidi ya miaka
20 iliyopita, lakini sasa tumeweza kukutana tena ingawaje siyo wote laakini kwa
kuwa lengo letu ni moja tuna amini na wengine watakuja taratibu” amesema .
Mmoja wa wajumbe wa UWKS Mbunge wa Kigoma
Mjini Zito Kabwe(ATC) amesema tuliopo ni wajumbe 18, imefanyika kazi
kubwa kutafutana lakini naamini kila mmoja wetu atabeba jukumu la kuwavuta
wengine hadi darasa litatimia.
Kabwe ambaye ni ameweka wazi kuwa Umoja
huo utapeleka msaada katika shule hiyo kwa kuwa imechakaa na kurekebisha baadhi
ya miundombinu iliyochakaa kwa kuwa wakati wao wakisoma walikuta maabara
zikifanya kazi lakini kwa sasa zimechakaa, hiyo ni kama kurudisha shukrani kwa
jamii.
Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari
Kigoma kuanzia 1991 -1994 (UWKS) umetokana na kikao cha wanajumuiya cha tarehe
06 Machi 2011ambapo ndipo lilipopatikana wazo la kuwa na Umoja huu ndipo
wajumbe walipo azmia kuanza mchakato wa kusajili Umoja huo ambao leo
umezinduliwa rasmi. Wajumbe waliojiorodhesha idadi yao inafikia 40 mapaka sasa.
Post a Comment