Ads

TAKUKURU IMEOKOA KIASI CHA SH. BILIONI 4 NA KUREJESHWA KWA WAKULIMA

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa( TAKUKURU) imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 4 na kurejeshwa kwa wakulima na vyama vya Ushirika. Akizungumza na wanahabari katika ofisi za makao makuu TAKUKURU, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo , Brig.Jen.John Mbungo amesema kuwa TAKUKURU imefanikiwa kuokoa kiasi hicho ambacho baadhi zimerejeshwa kwa wakulima na vyama vya Ushirika ama kutunzwa katika akaunti maalumu zilizofunguliwa kwa ushauri wa warajisi wa vyama vya ushirika na wakuu wa mikoa na wilaya kwa ajili ya kuzirejesha kwenye vyama vya ushirika ama wakulima.

No comments