DC LYANIVA : WALEZI WAZAZI MSIKWEPE WAJIBU WENU.
Mkuu wa
Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaniva
akionesha DVD ya nyimbo ya wato
yatima katika kitu cha Amani Foundatio cha Kigamboni Jijini Dar es salaam
alipokwa akiizindua na kuweka jiwe la msingi
na kuendesha harambee ya ujenzi wa kituo hicho ,anayefuata upande wa kulia ni Rahel mhando , Katibu Tawala Wilaya ya Kigamboni ,anayefuata upande wa kushoto ni Zubeida Makame Mkurugenzi wa kituo cha Amani (Picha na John Luhende).
Mwamba wa habari
Wito
umetolewa kwa wazazi nalezi kutimiza
wajibu wao kwa kuwaleo watoto badala ya
kuwaacha bila uangalizi jambo ambalo
limesababisha kuwa na watoto wasio na makazi maalumu.
Wito huo
umetolewa na na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Felix Lyaniva wakati alikizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katika harambee ya kuchangia ujenzi na uwekaji jiwe lamsingi ujenzi wa Kituo cha Amani cha kulelea watoto
yatima kilichopo kibugumo Kigamboni Jijini Dar es salaam, na kuogeza kuwa kutekeza
watoto ni dhambi kwa Mungu .
‘’Mtu ambaye
anaacha familia yake na kuitelekeza na kuiacha ikihangaika huyo hata pata
thawabu kwa Mungu ,kufanya hayo ni
kukwepa wajibu ,napia wenye vituo hivi vya yatima naomba visiwe kwa faida ya mtu mmoja bali vifaidishe watoto na jamii”alisema
Jambo hili
la kutelekeza watoto na kuwaacha mitaani linafanywa na baadhi ya wana jamii limekemewa pia na Katibu tawala Wilaya ya Kigambo
Rahel Mhando ambapo ameitaka jamii kujiukiza na kuchukua hatua najukumu kwa
watoto hao.
“Kwanini
tunasema wanaoishi katika mazingira magumu wakati wana koo na familia zao walikotoka?jamii kwa namna
moja amanyingine lazima itoe ushirikiano
kuhakikisha hawa watoto wanapata huduma
tena sisi ni waumini wazuri kilasiku kanisani msikitini lakini huyo
mtoto mmoja wa ndugu yako amekushindaje?Alihoji
Kwaupande
wake Mkurugenzi wa kituo hicho Zubeida Makame
, amwataka wanandoa kuishi kwa maelewano ili kuepuka mafarakano ya
kifamilia ambayo yamesababisha watoto kuishia mitaani, na kusema kuwa yeye
anatoa huduma kwa watoto hao na kwamba
hajipatii faida .
‘’Malipo ya
kazi hii ni kwa mwenyezi Mungu peke yake maana hii siyo biashara,malezi haya ni
wito naombatu familia ziwe na uvumilivu ili walee wato wao walinde sana ndoa
zao ili waishi vizuri na watoto wao wasifarakane ”alisema
Kituo cha
Amani kina watoto zaid ya 50 , Majengo ya kituo hicho ili yaweze kukamilika
jumla ya shigi milioni miamoja sabini na tano lakisaba na sabini elfu,lakini
pamoja nakuendeshwa harambee hiyo Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul
Makonda ameahidi kumalizia ujenzi huo.
Post a Comment