Ads

Mbunge Viti Maalum Anatropia atoa elimu ya mikopo


Mbunge wa viti maalum MANISPAA ya Ilala Anatropia Theonest akizungumza na Wanawake wa Buguruni kwa Mnyamani Dar es Salaam jana wakati wa kutoa Elimu ya Mikopo kwa Wanawake wa Jimbo la Segerea ambapo ufunguzi wake ulikuwa Mnyamani (Picha na Heri Shaban)

Mwambawahabari
Na Heri Shaban
MBUNGE wa Viti Maalum Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ANATROPIA Theonest atoa mafunzo ya elimu ya mikopo kwa Wanawake wa kata ya Buguruni Mnyamani.

Mafunzo hayo endelevu kwa Wanawake wa Jimbo la Segerea yameanza leo ambapo mbunge huyo ameshirikiana na Benki ya DCB kwa lengo la Kuwapa elimu Wanawake hao waweze kuchukua mikopo kupitia benki hiyo.


Anatropia alisema dhumuni la semina hiyo ni kuwajengea uwezo Wajasiriamali watakaochukua mikopo watumie kwa malengo yaliokusudiwa.


"Wanawake wa Jimbo la Segerea mshikamane mchangamkie fursa hii mikopo hii kwa sasa aina riba DCB wameondoa vikwazo tofauti na awali "alisema Anatropia.

Ametaka Wanawake wajikwamue kiuchumi washikamane wawe wamoja wachukue mikopo kwa wakati waweze kufanya biashara mbali mbali ikiwemo ya ufugaji kuku.

Alisema elimu hiyo itawawezesha kupanua wigo katika sekta ya biashara watajifunza kuuza bidhaa ambazo zinaingiza fedha kwa wakati ili waweze kuwekeza.


Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ina Kata 36 atakikisha elimu hiyo inafika kwa walengwa katika kata zote za Manisipaa Ilala.


Alisema Mpango huo wa utoaji wa Elimu ya mikopo kwa Wanawake ambao umezinduliwa  utawafikia kata zote ili wakikopa fedha za mkopo wajue matumizi yake katika kukuza mitaji.

Kwa upande wake Ofisa wa Benki ya DCB Ukonga Hamis Mwisomba alisema mikopo inatolewa kwa vikundi vya watu watano watano ambao wanafamiana.

Mwisumba alisema sharti lingine kwa wakopaji kuanzia miaka 18 hadi 36 na kabla kuchukua mikopo hiyo watapatiwa elimu nyingine kupitia vikundi vyao.

Aliwataka wakopaji wafamiane wasiwe ndugu wala familia
Moja na wakikopa wakumbuke marejesho


Naye Katibu Kata wa Kimanga wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Aristide Ndyamukama aliwataka Wanawake washirikiane na MBUNGE wao ili wafikie malengo waliokusudia na wakikopa warejeshe kwa Wakati ili na wengine waweze kukopa fedha hizo

No comments